Habari

MVUA KUBWA KUENDELEA KUNYESHA HADI MWISHO MWA MWEZI APRIL

     Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzaniaa TMA imesema kipindi cha Mvua kubwa kinatarajiwa kuendelea hadi Mwisho wa Mwezi huu huku ikiwataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua hizo.

   Akizungumza na ZBC Mchambuzi wa Hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bi.Rose Senyangwa amesema Mvua hizo zinatarajiwa kupungua kuanzia Mwanzoni mwa Mwezi Mei Mwaka huu.

IDADI KUBWA YA MADARAJA YAATHIRIKA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA

     Mvua zinazoendelea kunyesha Maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro kuanzia Mwishoni mwa  Mwezi March zimesababisha kuathirika kwa Miundombinu ya Barabara pamoja na Madaraja 9 kutoka Maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro .

ZIPA NA SINGAPORE KUIMARISHA UWEKEZAJI

    Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Zipa imekutana na Balozi wa Singapore Nchini Tanzania Balozi Douglas Foo aliefika kwa ajili ya  kujitambusha.

    Akizungumza na Balozi huyo Mkurugenzi mipango na utafiti Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Alhaji Mtumwa Jecha amesema hatua hiyo itafungua fursa za uwekezaji Zanzibar kutoka Nchini  Singapore, ukizingatia Nchi zote ni za Visiwa

SEREKALI KUDHIBITI MIANYA YA RUSHWA NA KUONGEZA UWAJIBIKAJI.

    Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema mafanikio makubwa yatapatikana katika kudhibiti mianya ya Rushwa na kuongeza kasi ya Uwajibikaji endapo Wataalamu wa Kamati za kuchunguza hesabu za Serikali za Mabunge ya Sadcopac zitatekeleza ipasavyo.

   Akifunga Mafunzo hayo Mhe. Majaliwa amesema ili lengo la Mafunzo hayo yaweze kufikiwa ni vyema kwa  Washiriki hao kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika Taasisi zao na kudhibiti Rushwa na kusimamia haki na uwajibikaji ili kuimarisha  Utawala bora.

RAIS SAMIA ATUKUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA UDAKTARI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Nchini Uturuki.

     Rais Dkt.Samia ametunikiwa Shahada hiyo na Mkuu wa Chuo Kikuu Ankara cha Nchini Uturuki na Profesa Necdet Unuvar kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo ambapo Rais Samia yupo katika Ziara kazi ya Siku Tano Nchini humo.

MAFUNZO KWA KAMATI ZA SADCOPAC YATASAIDIA KUFANIKISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kufanyika kwa Mkutano wa kutoa Mafunzo ya kuzijengea uwezo Kamati za kuchunguza hesabu za Serikali za Mabunge ya Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kutasaidia kuchochea kasi ya maendeleo kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

WAZIRI MKUU AMEOMBA USHIRIKIANO KWA WANAOKUSANYA MAONI YA DIRA MPYA YA TAIFA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, amewataka Wakuu wa Mikoa Tanzania Bara na Zanzibar kutoa ushirikiano kwa Timu za Wataalamu wanaokusanya maoni ya Dira mpya ya Taifa katika Mikoa yao ili waweze kupata maoni yenye tija kwa Taifa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo  Jijini Dodoma wakati akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara na Zanzibara kuelekea Mchakato wa utoaji Maoni ya Dira ya Taifa ya maendeleo.=

Aidha amewataka kushirikiana na Viongozi wa Dini ili kuweza kufanikisha zoezi hilo la ukusanyaji maoni kwa Wananchi.

SERIKALI KUIMARISHA USAFIRI WA BARABARANI

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Serikali inaimarisha Sekta ya usafiri wenye uhakika na salama ili kuondosha usumbufu kwa Wananchi.

Akifungungua Mkutano juu ya usalama wa usafiri, Dkt. Khalid amesema uimarishaji huo unaenda pamoja na uimarishaji Miundombinu ya Barabara ili kupunguza Ajali na Msongamano pamoja na kupunguza gharama.

SERIKALI KUTUNGA KANUNI MPYA ZA UTUNZAJI MAZINGIRA

Serikali ipo Mbioni kutunga Kanuni mpya za utunzaji wa Mazingira kwa Wazalishaji wa Vinywaji vinavyotumia Chupa za Plastiki na Vifungashio ambapo Watalazimika kukusanya Chupa zilizotumika kutoka Mitaani kwa lengo la kutunza Mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo,ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Akifungua Kikao cha Majadiliano na Wazalishaji wa Bidhaa zinazofungashwa kwa Plastiki kilichohusu kupata Ufumbuzi wa tatizo Kuzagaa kwa Chupa za Plastiki Mitaani. 

KAMISHENI YA ARDHI IMEOMBWA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA HATI MILIKI

Kamisheni ya Ardhi Pemba imeombwa kusaidia upatikanaji wa haraka hati miliki, katika maeneo ambayo yameainishwa kwenye utekelezaji wa Mradi wa ukuzaji Uchumi Jumuishi Zanzibar (Big-Z) Pemba.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa Big-Z upande wa Pemba Ali Salum Ali, kwa nyakati tafauti wakati wa ziara ya kamati ya usimamizi wa Mradi upande wa Pemba.

Amesema miongoni mwa vigezo muhimu wakati wa utekelezaji wa Mradi huo, kutoka kwa Wafadhini ni kwamba Ardhi inayotumika inatakiwa iwe haina Migogoro yoyote.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.