Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Zipa imekutana na Balozi wa Singapore Nchini Tanzania Balozi Douglas Foo aliefika kwa ajili ya kujitambusha.
Akizungumza na Balozi huyo Mkurugenzi mipango na utafiti Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Alhaji Mtumwa Jecha amesema hatua hiyo itafungua fursa za uwekezaji Zanzibar kutoka Nchini Singapore, ukizingatia Nchi zote ni za Visiwa
Akizitaja Miongoni mwa fursa hizo amesema kuwa ni pamoja na Wafanyakazi kujifinza uzowefu hasa ukizingatia uwepo wa Kituo kimoja cha Uwekezaji kuwa na mfumo wa maombi yanayorahisisha shughuli hizo Dunia nzima
Nae Balozi wa Singapore Nchini Tanzania Balozi Douglas Foo amesema kwa sasa wameanzisha Taasisi maalum za kutatua Migogoro ya Uwekezaji Nchini Singapore kinachoshughulikia migogoro ya Uwekezaji kabla ya kufikishwa Mahakamani jambo ambalo limeipatia Umaarufu Nchi hiyo katika Uwekezaji
Aidha, Balozi Foo amesema Singapore imefanikiwa kuwekeza katika Elimu kwa kuwasomesha ili kuwaandaa Wananchi wake kulitumikia Taifa lao hivyo Zipa iandae Program ya maeneo wanayotaka kujifunza na Singapore kupitia Balozi yake Nchini Tanzania itatoa mashirikiano ya kufanikisha hilo.