Waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Ruvuma chini ya Taasisi ya 'JAI' Tanzania wamejitokeza kuchangia damu safi na salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya taasisi hiyo kitaifa ambapo ufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Mratibu wa Huduma Salama Mkoa wa Ruvuma Fredrick kihaule amewashukuru wachangiaji damu wote waliojitokeza kuchangia damu kwani wamegusa kwa kiwango kikubwa sana cha mahitaji ya damu katika hospitali ya Mkoa.
Nae, Makamu Katibu wa JAI Mkoa wa Ruvuma Ndugu Abdulwahidi Thabit Kajundira ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwani hakuna kiwanda cha kutengeneza damu na wala haiuzwi hivyo lazima damu itoke kwa binadamu mwingine.
stories
standard