Wananchi wametakiwa kutumia fursa za ujasiriamali zinazopatikana katika Maeno yao ili kujikwamua Kiuchumi kwa shughuli wanazozifanya.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh.Zuberi Ali Maulid amesema hayo katika Uzinduzi wa Soko la Wajasiriamali Wananwake Fujoni lilojengwa kwa Mfuko wa Maendleo wa Muwakilishi wa Jimbo Bumbwini.
Amesema Wananchi wanatakiwa kuthamini juhudi za Viongozi za kuwaletea maendeleo na kuwakwamua na umasikini Mh.Zuberi amewashauri kuitunza Miundombinu ya Soko hilo ili idumu kwa Muda Mrefu.
Mbunge wa Jimbo na Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini wamewashauri Wanawake watakaotumia Soko hilo kuhakikisha wanafanya usajili wa Vikundi vyao.
Nao Wanawake katika Soko hilo Jipya wamesema kuwa litawasaidi kufanya Kazi zao katika Sehemu rasmi.
Akizungumzia Fedha za Mifuko ya Mbunge na Mwakilishi Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kaskazini 'b' Abdulrahman Ali Muhtar amesema Fedha hizo zinatumika Miradi ya Kijamii katika kuwaondoshea matatizo yao.