Akifunga Mafunzo hayo Mhe. Majaliwa amesema ili lengo la Mafunzo hayo yaweze kufikiwa ni vyema kwa Washiriki hao kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika Taasisi zao na kudhibiti Rushwa na kusimamia haki na uwajibikaji ili kuimarisha Utawala bora.
Kwa vitendo uwezo waliojengewa , mbinu na maarifa waliyoyapata kupitia Mafunzo ya Siku Mbili ya Jumuiya ya Sadcopac yaliyofanyika Nchini.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ametumia fursa ya Mkutano huo kuwahamasisha Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Sadcopac kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini na kuwa Mabalozi wazuri wa kuitangaza Zanzibar watakaporejea katika Mataifa yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo wamesema wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo kubadilishana Mawazo na uzoefu kutoka kwa Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni " kujenga uwezo wa kudhibiti Rushwa, uwajibikaji na uwazi katika Maliasili kwa Wajumbe wakati za hesabu za Umma (PCA) Kamati zinazofanana nazo na Wataalamu