Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzaniaa TMA imesema kipindi cha Mvua kubwa kinatarajiwa kuendelea hadi Mwisho wa Mwezi huu huku ikiwataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua hizo.
Akizungumza na ZBC Mchambuzi wa Hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bi.Rose Senyangwa amesema Mvua hizo zinatarajiwa kupungua kuanzia Mwanzoni mwa Mwezi Mei Mwaka huu.
Kuhusu Utabiri wa Mwelekeo wa Mvua za Masiki kwa kipindi cha Marchi hadi Mei 2024 Bi.Rose amesema walichotabiri ndicho kinachoendelea kutokea kwa sasa kama hapo anavyoeleza.
February Mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa Utabiri wa Mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Maeneo yanayopata Misimu Miwili ya Mvua kwa Mwaka ambapo zilitarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani