Kamisheni ya Ardhi Pemba imeombwa kusaidia upatikanaji wa haraka hati miliki, katika maeneo ambayo yameainishwa kwenye utekelezaji wa Mradi wa ukuzaji Uchumi Jumuishi Zanzibar (Big-Z) Pemba.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa Big-Z upande wa Pemba Ali Salum Ali, kwa nyakati tafauti wakati wa ziara ya kamati ya usimamizi wa Mradi upande wa Pemba.
Amesema miongoni mwa vigezo muhimu wakati wa utekelezaji wa Mradi huo, kutoka kwa Wafadhini ni kwamba Ardhi inayotumika inatakiwa iwe haina Migogoro yoyote.
Meneja huyo wa amesema Miradi yoyote watahakikisha baada ya Miezi Minane watakua wameshakamilisha Michoro na kuanza zoezi la ujenzi wake ili iweze kumalizika kwa wakati.
Nae mkadiriadi Majenzi Daimon Richard, amesema tayari wameshakabidhiwa maeneo mbali mbali yanayotaka kutumika kwenye Ujenzi wa Mradi huo.
Injinia wa Baraza la Maji Wete Said Abdalla Said, amesema walikua na kiu kubwa juu ya ujio Watendaji kukagua maeneo mbali mbali yaliopo chini ya Baraza hilo.
Ziara hiyo ya ukagazi wa maeneo yatakayotekelezwa na Miradi wa Big-Z, imekamilika kwa Wilaya zote Nne za Pemba, Wete, Micheweni, Chake Chake na Mkoani.