Habari

KAMATI MAWASILIANO YAFURAHISHWA NA UFANISI WA TCCA

    Kamati ya Mawasiliano Ardhi na  Nishati ya Baraza la Wawakilshi imesifu hatua iliyofikiwa katika uendeshaji na usimamzi wa Viwanja vya Ndege Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuimarika usalama  wa Usafiri wa  Anga Nchini.

     Akizungumza walipotembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania wakiongozana na Watendaji wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Yahya Rashid Abdallah amesema usalama wa Anga unatakiwa kupewa kipaumbele  ili kuiwezesha Anga kuwa salama na kuleta tija.

SMZ NA SMT KUSHIRIKIANA KUENDESHA KIWANDA CHA KUCHAKATA MWANI

   Katika Kipindi cha Miaka 60 ya Muungano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kushirikiana na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kuendesha Kiwanda cha Kuchakata Mwani kilichopo Zanzibar chenye uwezo wa Kuchakata Tani Elfu 30 kwa Mwaka kwa kuongeza upatikanaji wa malighafi ya Mwani kutoka Tanzania Bara.

    Hayo yamesemwa Jjijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Khamis Ulega wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika Kipindi cha Miaka 60 ya Muungano.

WADAU WATAKIWA KUONDOSHA URASIMU SEKTA YA ELIMU

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Meh.Leila Mohammed Mussa amewataka Wadau wa Elimu waliohudhuria Mkutano wa 7 wa mabadiliko ya Elimu kwa maendeleo endelevu kuhakikisha urasimu hauchukui nafasi katika uboreshaji wa Sekta ya Elimu Nchini

    Ameyasema hayo huko Hoteli ya madinatul Bahri Mbweni, Waziri huyo amewataka Wadau hao kujadili matatizo yaliopo katika Sekta hiyo pamoja na kuyatafutia ufumbuzi.

   Aidha amehimiza suala la uwajibikaji kwa Vitendo katika mapendekezo watakayokubaliana kwenye Mkutano huo.

AINA MPYA YA MICHE YA MIGOMBA KUANZA KUTUMIKA ZANZIBAR

   Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kutumia aina mpya ya Miche ya Migomba aina Malindi iliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Mbogamboga na Matunda Taha Mkoani Arusha ili kuondoa tatizo la Uagizaji wa zao hilo kwa fedha nyingi.

    Hayo yamebainika Wakati wa Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii ya Baraza la Wawakishi Zanzibar katika Taasisi ya Mboga Mboga iliyopo Mkoani Arusha iliyolenga kujifunza mbinu bora za Kilimo.

WAZIRI MASOUD AMETAKA MIRADI YA 2023/24 IKAMILISHWE NA IANZE KUTUMIKA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed, ameitaka Kamati ya Uongozi ya Ofisi yake, kuhakikisha Miradi ya Mwaka 2023/24 iwe imekamilishwa na ianze kutumika.

   Akizungumza na Kamati hiyo ya Uongozi katika Ukumbi wa Makao Makuu ya KVZ Mtoni amesema kukamilika kwa Miradi hiyo kutatoa nafasi ya utekelezaji wa Miradi mipya iliyobuniwa  ambayo itawalenga Wananchi kwa  kuendeleza shughuli zao kwa kujiongezea Kipato na kukuza pato la Nchi.

SERIKALI YAJA NA MPANGO MPYA KWA USAFIRI WA VYOMBO VYA BAHARINI

     Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohammed amewataka Wadau wa Mkutano wa Kikanda juu ya usalama wa Vivuko Afrika kutoka na mkakati ambao utasaidia kuweka hali ya usalama wa vyombo vidogo vidogo vya Baharini, Ziwani na Mtoni ili kuweza kupunguza ajali zinazotokana na Vyombo hivyo katika Bara la Afrika.

RAIS SAMIA ANATARAJIWA KUANZA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI UTURUKI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza Ziara ya Kiserikali Nchini Uturuki ikiwa ni hatua ya kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya Tanzania na Uturuki.

WATUMISHI OR TMSMIM KUZINGATIA KANUNI ZA UTUMISHI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohammed, amewasisitiza Watumishi wa umma kuwa mfano bora katika kufata misingi na kanuni za Kiutumishi.

 akizungumza na Watendaji wa Ofisi Kuu Ofisini kwake Vuga, ameitaka kila Idara kuhakikisha inajitathmini na kuchukua hatua katika Utendaji wa kazi ili kuweza kufikia malengo bora ya kiutendaji yaliyokusudiwa.

SMZ KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia  kuimarisha Sekta ya Elimu kwa Unguja na Pemba

Akizungumza hayo katika Ziara ya kuangalia maendeleo ya  Mradi wa Skuli za Sekondari zinazojengwa Mfenesini na Gamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhamed Mussa ameasema  kuwa Skuli zinazojenga zitaweza  kuleta Mageuzzi makubwa ya Elimu.

WAKULIMA WA MWANI MUUNGONI WAMEKABIDHIWA BOTI

Uzalishaji wa Mwani katika Kijiji cha Muungoni Wilaya ya Kusini Unguja unatarajiwa kupanda kutoka Tani Kumi hadi 20 kwa kila Bamvua kutokana na Kulima Kitaalamu pamoja na kuwa na Nyenzo za Kisasa zinazorahisisha shughuli hiyo.

Wakaazi wa Kijiji cha Muungoni ambacho mashuhuri kwa Kilimo cha Mwani wakizungumza kufuatia msaada wa Boti waliyopatiwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na Mazingira TNC, wameeleza matarajio yao baada ya Boti hiyo ni kuongeza uzalishaji.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.