Habari

TUME YA KUSHUGHULIKIA HOJA ZA MUUNGANO KUUNDWA

       Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye nyanja zote za Maendeleo, Kisiasa, Uchumi, Utamaduni na huduma za Jamii yameipatia Nchi heshima kubwa kwenye Jumuiya ya Kimataifa. 

    Dk. Mwinyi ameyasema hayo Viwanja vya Maonesho ya Biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharibi 'b' Wakati wa Uzinduzi wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

SMZ YATHAMINI JUHUDI ZINAZOFANYWA NA WAWEKEZAJI

    Serikali inathamini  juhudi zinazofanywa na Wawekezaji za kuwekeza katika Maeneo ya Visiwa vya Zanzibar ambayo yanaleta tija katika Jamii.

    Waziri wa Nchi Oisi ya Makamo wa Pili wa Rais Sera uratibu na Baraza la Wawakilishi Mh.Hamza Hassani Juma amesema hatua ya kuweza katika Sekta mbalimbali imekuwa ikileta tija kwa Serikali kwani husaidia kuongeza Pato la Taifa .

POLISI NCHI 14 KUFANYA MAFUNZO KUKABILIANA NA UHALIFU

      Jeshi la Polisi Nchini linatalajia kuwa, Mwenyeji wa Mafunzo ya utayari kwa vitendo Mwaka huu yatakayo jumuisha Nchi 14 Wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi ukanda wa Mashariki mwa Afrika  Eeapcco April 13 Hadi 18.

    Akitoa Tarifa Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi David Misime amesema  Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi ambapo  Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Vyeo mbalimbali Wapatao 670 wanatarajiwa kushiriki.

TULIA TRUST YAREJESHA FURAHA KWA MJANE MBEYA

 

   Taasisi ya  Tulia Ttrust imetoa msaada wa kumjengea Nyumba ya kuishi Mama Mjane  Singwava Jackson kwa lengo la  kumpunguzia shida na Familia yake.

    Akikabidhi Nyumba hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust Dkt. Tulia Ackson  amesema Taasisi yake itaendelea kusaidia Jamii hasa Watu wenye mazingira magumu

WAISLAM KUENDELEZA MEMA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al haj Dkt Huseein Mwinyi amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendeleza mema waliyodumu nayo katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuimarisha ustawi wa Jamii.

Akizungumza katika hafla ya Baraza la Eid huko Ziwani amesema kufanya hivyo kutaweza kuidumisha Nchi katika hali ya Amani na Usalama.

ZANZIBAR YAUNGANA NA WAUMINI WENGINE KUSHEREHEKEA EID FITRI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haj Dkt Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika ibada ya Sala ya Eid Fitri katika Msikiti wa Jamiiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.

Akitoa Khutba ya Eid El fitri Khatib wa Sala hiyo Sheikh Abdulkarim Said Abdul amewahimiza Waumini wa dini ya Kiislam kuendeleza huruma, upole kama funzo linalotokana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 

Amesisitiza umoja na mshikamano baina ya Waislam ili Nchi iweze kupata maendeleo zaidi. 

MAMA MARIMA MWINYI KUWAPA SADAKA YA EID WATOTO YATIMA NA WAZEE

Mke wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariam Mwinyi amevitembelea Vituo vya kulelea Watoto Yatima pamoja na Nyumba za Wazee wasio jiweza kwa kuwapa sadaka ya Eid Fitri.

Akizungumza na Watoto hao Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Mwenyekiti wa Maisha bora Foundation amesema katika kuwajali Watoto Kivitendo Serikali imekuwa nao Karibu kuhakikisha wanasherehekea Sikukuu kwa Utulivu na kuwataka Watoto hao kuendeleza Maadili mema waliojifunza kipindi cha Mwenzi wa Ramadhani.

VIJANA WAMEONYWA DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaj Hassan Kabeke, amekemea tabia ya baadhi ya Vijana kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya, ikiwemo Mirungi na Mihadarati, zinazotajwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa na kudhoofisha Afya zao

Alhaj Kabeke ametoa onyo hilo katika Hutba ya Eid El Fitri katika Swala ya Eid iliyoswaliwa Kimkoa katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza kufuatia kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mojawapo ya Nguzo kuu ya Dini ya Kiislamu.

JUMLA YA WATOTO 11 WAMEZALIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MNAZI MMOJA KUAMKIA USIKU WA SIKUKUU

Jumla ya Watoto 11 wamezaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja ikiwemo Wanawake Watano na Wanaume 6 kuamkia Usiku wa  Skukuu ya Iddilftri.

Akizungumza na ZBC Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Aziza Khatib Abdallah amesema Wazazi wote waliojifungua Watoto hao wanaendelea vizuri amewaomba viongozi kuwasaidia kuwatatulia matatizo yanayowakabili katika Hospitali hiyo ikiwemo kuwaongezea Vitanda kwa ajili ya Wazazi wanaofika hapo.

SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    Serikali imesema itaendelea kutoa msaada kwa Wanchi ili kuwawezesha kiuchumi.

     Akizungumza katika Makabidhiyano ya Gesi  huko Raha Leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi , Uchumi na  Uwekezaji Mhe Sharif Ali Sharif amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha Wananchi kujikimu kimaisha na kupunguza Matumizi ya Makaa na kuni ili kutunza mazingira na kuwa na Afya Njema. 

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.