Habari

SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

    Serikali imesema itaendelea kutoa msaada kwa Wanchi ili kuwawezesha kiuchumi.

     Akizungumza katika Makabidhiyano ya Gesi  huko Raha Leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi , Uchumi na  Uwekezaji Mhe Sharif Ali Sharif amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha Wananchi kujikimu kimaisha na kupunguza Matumizi ya Makaa na kuni ili kutunza mazingira na kuwa na Afya Njema. 

ZBC YAWATAKIA WAISLAMU KHERI YA EID EL-FITR

     Shirika la Utangazaji Zanzibar linawataka Waislamu wote Nchini Kheri ya Sikukuu ya Eid  al-fitri, na Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumaliza salama Mfungo wa  Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 

    Mwenyezi Mungu Atakabaal Dua zetu na Swaumu zetu , Na aendelee kutudumishia Amani katika  Taifa letu , Umoja na Mshikamano , katika misingi ya kufanya yaliyo mema .

    Tunawatakia Kheri  na Baraka za Sikukuu ya Eid El-fitr 

MBUNGE JIMBO LA KWAHANI AZIKWA KIJIJINI KWAO MUYUNI

      Wakati huohuo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki katika Maziko ya Mbunge wa Jimbo la Kwahani Marehemu Ahmada  Yahya Abdulwakil yaliyofanyika Kijijini kwao Muyuni.

     Akisoma Wasifu wa Marehemu Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mjini Awadh Haji amesema Marehemu atakumbukwa kwa namna alivyokuwa akishirikiana na Viongozi wengine kuwaletea Wananchi Maendeleo.

RAIS MWINYI ASHIRIKI MAZIKO YAMAREHEMU BURHANI SAADAT

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Viongozi wengine ameshiriki Maziko ya aliyekuwa Waziri wa Zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Burhani Saadat Haji yaliyofanyika Makaburi ya Kiembesamaki.

     Marehemu Saadat aliefariki Jana Nyumbani kwake kwa Mchini Wilaya ya Magharib ‘b’ amesaliwa Msikiti wa Maisara na baadae kuzikwa Makaburi ya Kiembe Samaki Mkoa wa Mjini Magharib.

WIZARA YA ARDHI IMESITISHA UJENZI KWENYE SHAMBA LENYE MGOGORO SHAKANI

Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma amesimamisha shughuli zote zikiwemo Ujenzi katika Shamba liliopo Shakani Minazini Wilaya ya Magharibi  kutokana na Shamba hilo kuwa na mgogoro.

Naibu Waziri huyo akiwa katika Ziara maalum kufuatia kupokea malalamiko ya mgogoro wa Shamba hilo amekutana na kukutana na pande zenye Mgogoro na hatimae kufikia maamuzi ya kusitiza shughuli zote hadi litakapotoka agizo jengine huku akiwasihi Wananchi kuacha kuuziana Ardhi kienyeji.

WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE NIA NJEMA YA KUULINDA MUUNGANO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, amezindua nembo na kauli mbiu ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku akiwataka Watanzania kuutumia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu kuchagua Viongozi wenye nia njema na Muungano.

Mhe. Kassim Majaliwa, ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo hiyo  ambapo amewataka Watanzani kuulinda Muungano huo.

 Majaliwa amewataka Watanzania wote, Bara na Visiwani kundelea  kuulinda, kuuenzi, kujivunia na kuuthamini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

MPANGO WA MAGEUZI WA SEKTA YA ANGA

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk Khalid Salum Mohammed amesema kupitia mpango wa mageuzi ya Sekta ya Anga Serikali imeweza kupata mafanikio makubwa ya kiuchumi kufuatia kuimarika kwa huduma muhimu kwa Abiria

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusiana na maendeleo ya Sekta ya Anga Nchini amesema mabadiliko hayo yanayotokana na mipango imara ya Serikali yanayolenga kukuza uchumi kupitia utowaji huduma bora zinazokwenda na wakati na kusababisha kupata tunzo ya uwanja bora barani Afrika

ZURA IMETANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA YA PETROL KWA MWEZI HUU.

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), imetangaza Bei mpya za Mafuta ambapo Mafuta ya Petrol, Disel na Mafuta ya Ndege yameendelea kupanda kwa Mwezi huu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari katika Ofisi ya Mamlaka hiyo Maisara Meneja kitengo cha Mahusiano Mbaraka Hassan Haji, amesema Bei ya Mafuta ya Petrol kwa Mwezi huu itakuwa ni Shilingi 3,133 kutoka Shilingi 3,118 ya Mwezi uliopita.

SERIKALI IMEWAONYA WAFANYABIASHARA WA SUKARI WANAOKIUKA BEI ELEKEZI

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban amewaonya baadhi ya Wafanya Biashara Kisiwani Pemba wanaendelea kuwauzia Wananchi Bidhaa za Vyakula ikiwemo Sukari kinyume na Bei elekezi ilowekwa na Serikali.

Waziri Omar ametoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Wafanya Biashara Masheha na Watendaji wa Wizara hiyo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha utoa wa huduma ya usajili wa Biashara na Mali BPRA Mjini Chake Chake.

Amesema licha ya Serikali kutoa bei elekezi ya bidhaa ya Sukari lakini kuna baadhi ya Wafanya Biashara wamekuwa wakikiuka sheria.

WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUHAMIA MASOKO MAPYA YATAKAPOKAMILIKA

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mh Masoud Ali Mohammed,  amewataka Wafanyabiasha waliopo katika Masoko ya muda, kuhamia katika Masoko mapya mara yatakapokamilika kujengwa.

Akizungumza na Kamati ya Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe ambayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni, ameagiza kupewa kipaumbele katika masoko mapya Wafanyabiasha waliokuwepo hapo awali na kufanya utaratibu wa kuwapatia nafasi Wafanyabiashara wengine.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.