Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Viongozi wengine ameshiriki Maziko ya aliyekuwa Waziri wa Zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba Burhani Saadat Haji yaliyofanyika Makaburi ya Kiembesamaki.
Marehemu Saadat aliefariki Jana Nyumbani kwake kwa Mchini Wilaya ya Magharib ‘b’ amesaliwa Msikiti wa Maisara na baadae kuzikwa Makaburi ya Kiembe Samaki Mkoa wa Mjini Magharib.
Viongozi wengine walioshiriki Maziko hayo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdalla, Marais Wastaaf Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na Dk. Amani Abeid Karume pamoja na Viongozi Wengine na Wananchi.
Marehem Saadat Alizaliwa Mwaka 1935 Kikwajuni katika uhai wake alishika Nyadhifa mbali mbali katika ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwemo Waziri wa Kilimo na Mifugo, Waziri na Mshauri Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Peponi Amina