WIZARA YA ARDHI IMESITISHA UJENZI KWENYE SHAMBA LENYE MGOGORO SHAKANI

NAIBU WAZIRI WA ARDHI

Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Salha Mohammed Mwinjuma amesimamisha shughuli zote zikiwemo Ujenzi katika Shamba liliopo Shakani Minazini Wilaya ya Magharibi  kutokana na Shamba hilo kuwa na mgogoro.

Naibu Waziri huyo akiwa katika Ziara maalum kufuatia kupokea malalamiko ya mgogoro wa Shamba hilo amekutana na kukutana na pande zenye Mgogoro na hatimae kufikia maamuzi ya kusitiza shughuli zote hadi litakapotoka agizo jengine huku akiwasihi Wananchi kuacha kuuziana Ardhi kienyeji.

Akizungumzia  kuhusiana na Shamba hilo Bi Salma Issa Khatib anadai kuwa Shamba hilo ni la kwake na amerithi kutoka kwa Marehemu Mume wake lakini cha kushangaza katokea Kijana anadai kuwa ni la kwake na kuanza kukata Viwanja kwa kuviuza huku Hamid Kirara anaedaiwa kuvamia Shamba hilo anadai kuwa ana vithibitisho halali vya eneo hilo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.