Habari

MHANDISI ZENA AKEMEA TABIA YA KUWAFUNGIA NDANI WATOTO WENYE ULEMAVU

      Serikali imesema hairidhiswhi na tabia ya baadhi ya Wazazi ya kuwafungia ndani Watoto wenye ulemavu wa akili kwani kunawakosesha haki zao za msingi.

     Rai hiyo ameitoa mara baada ya Iftar iliyoandaliwa na Taasisi ya Lulu Foundation huko Ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema hatua hiyo inasababisha kuikosesha Serikali Takwimu sahihi kwa Watoto hao kwa wanakosa haki zao wanazostahili ikiwemo Elimu afya pamoja na uangalizi mzuri wa Jamii.

TAHARUKI ! WANANCHI NGANA HATARINI KULIWA NA MAMBA

     Wananchi katika Kata ya Ngana Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wapo hatarini kuliwa na Mamba kufuatia Daraja la Mto Mwega kubomoka na kulazimika kuvuka kwa kuogelea ndani ya Mto huo unaosifika kuwa na Mamba wengi .

    Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mto huo umefurika Maji na kubomoa Daraja hilo,hali iliyopelekea kukata Mawasiliano ya upande Mmoja na mwingine ambapo Wananchi wameiomba Serikali kujenga Daraja hilo ili kuendeleza harakati zao

SERIKALI YATAKIWA KUONGEZA NGUVU KATIKA ZAO LA KOROSHO
WANANCHI KUENDELEA KUWAOMBEA DUA VIONGOZI WAO

      Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM kwa kushirikiana na Al-madrasat An -Nujuum ya Temeke Jijini Dar-es-salaam wamefanya Dua maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na

Viongozi wengine ili Mwenyezi Mungu awajaalie hekima busara katika Uongozi wao.

      Dua hiyo Maalumu imefanyika katika Ukumbu wa Karimjee iliyofanyika sambamba na ugawaji wa zawadi za vyakula kwa Vituo

DKT.MWINYI AONGOZA DUA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME

    Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi  amewaongoza Maelfu ya Wazanzibar katika Dua maalum ya Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume. 

    Dua hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini pamoja Wananchi imefanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni Kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Mzee Karume ambapo aliuawa Aprili 7,1972.      

WADAU ELIMU KUSHIRIKI KUPANGA MAENDELEO YA ELIMU

     Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewatka Wadau wa Elimu Nchini kushiriki kikamilifu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya Elimu na Program mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Elimu inaleta maendeleo kwa Mtu Mmoja Mmoja, Jamii na Taifa kwa Ujumla.

    Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati Akifungua Mkutano wa Mwaka wa pamoja wa Tathimini wa Sekta ya Elimu kwa Mwaka 2023/24  kwa Niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda

RIBA BOT YAPANDA SABABU MWENENDO WA UCHUMI WA DUNIA

   Benki Kuu ya Tanzania  BOT  imepandisha Riba kutoka Asilimia 5.5 iliyotumika  katika Robo ya Kwanza ya Mwaka hadi asilimia 6 ambayo itatumika katika Robo ya Pili ya Mwaka kuanzia Mwezi April hadi Juni 2024.

WAFANYABIASHARA WALIA NA UCHELEWESHWAJI WA USHUSHAJI WA MIZIGO BANDARINI

     Wafanya Biashara wa Nguo  wa  Maduka  ya Darajani wamelalamikia utaratibu mbovu wa ushushaji  wa mizigo yao  katika Bandari  ya Malindi  Jambo  ambalo kuzorotesha  shughuli za Kibiashara.

    ZBC imefika hadi  Shirika la Bandari la Zanzibar na kuzungumza na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  wa Shirika hilo  juu  ya malalamiko  ya Wafanya Biashara hao .

WANANCHI WAMETAKIWA KUHUDHURIA SALA NA BARAZA LA EID

    Ofisi ya Mufti Zanzibar imewaomba Wananchi kuhudhuria katika Ibada ya  sala ya eid na baraza la eid ili kusikiliza nasaha na Miongozo itakayotolewa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussen Ali Mwinyi.

    Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Khalid Ali Mfaume amesema Siku ya Eid ni muhimu kukumbushana mambo yanayohusu Dini ya Kiislamu na kukatazana mabaya ili kuepusha Jamii kwenda kinyume na Maadili yao

KATIBU ALAANI UHARIBUFU MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA MAJI

     Serikali imelaani Kitendo cha hujuma za kuharibu miundombinu ya huduma za Maji safi na salama katika  Visima vya Kidutani .

     Akizungumza katika kukagua athari za kuibiwa  Waya za Umeme  katika Visima  vya Maji huko Kidutani Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Ndg.Joseph John Kilangi  amesema wizi huo unarejesha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora karibu na makaazi yao . 

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.