SERIKALI YATAKIWA KUONGEZA NGUVU KATIKA ZAO LA KOROSHO

Zao la korosho

     Katika kuhakikisha , zao la Korosho linaongezewa thamani    katika   ubanguaji,   Wadau wa Zao hilo  wamesema Serikali inapaswa  kuongeza nguvu katika ubanguaji,ili kuondoka  na uuzaji wa korosho ghafi,  na kufikia lengo la Serikali la kubangua korosho zote zinazozalishwa  hapa Nchini ifikapo 2030.

    Wakizungumza katika Kikao cha Tathimini ya ubanguaji wa Korosho, baadhi ya Wadau kutoka katika Mikoa ya Lindi, Mtwara Ruvuma, Pwani na Tanga,  wamesema  Serikali inapaswa  kutoa Elimu  kwa Wakulima wa zao hilo,  ili kuongeza uzalishaji pamoja  kuunganisha vikundi vya  wabanguaji wadogo  wadogo.

      Alfred ni Mkururgenzi  Mkuu Bodi ya Korosho Tanzania, anakaelza mikakati waliyonayo ili kumhakikisha Mkulima wa Zzao hilo kuwa na soko la uhakika.

      Kwa mujibu wa Mkurugenzi Bodi ya Korosho amesema hali ya ubanguaji imeongezeka kutoka Tani  2000 kwa 2021, na kufikia Tani Elfu   26,600, kwa Mwaka 2023/2024.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.