TAHARUKI ! WANANCHI NGANA HATARINI KULIWA NA MAMBA

Daraja la Mto Mwega

     Wananchi katika Kata ya Ngana Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wapo hatarini kuliwa na Mamba kufuatia Daraja la Mto Mwega kubomoka na kulazimika kuvuka kwa kuogelea ndani ya Mto huo unaosifika kuwa na Mamba wengi .

    Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mto huo umefurika Maji na kubomoa Daraja hilo,hali iliyopelekea kukata Mawasiliano ya upande Mmoja na mwingine ambapo Wananchi wameiomba Serikali kujenga Daraja hilo ili kuendeleza harakati zao

    Kaimu Mkurugenzi Bi.Swaumu kumbisaga na Meneja Tarura Karimu Mtungata wamefika Eneo la Tukio na kujionea hali halisi na kulazimika  kuchukua Hatua za haraka 

    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela Katule Kingamkono amewasihi Wananchi kuwa Wavumilivu na Serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha Daraja linajengwa ili kuepusha athari za Binadamu kudhurika

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.