Wananchi katika Kata ya Ngana Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wapo hatarini kuliwa na Mamba kufuatia Daraja la Mto Mwega kubomoka na kulazimika kuvuka kwa kuogelea ndani ya Mto huo unaosifika kuwa na Mamba wengi .
Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Mto huo umefurika Maji na kubomoa Daraja hilo,hali iliyopelekea kukata Mawasiliano ya upande Mmoja na mwingine ambapo Wananchi wameiomba Serikali kujenga Daraja hilo ili kuendeleza harakati zao
Kaimu Mkurugenzi Bi.Swaumu kumbisaga na Meneja Tarura Karimu Mtungata wamefika Eneo la Tukio na kujionea hali halisi na kulazimika kuchukua Hatua za haraka
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela Katule Kingamkono amewasihi Wananchi kuwa Wavumilivu na Serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha Daraja linajengwa ili kuepusha athari za Binadamu kudhurika