Habari

SMZ WATHAMINI MCHANGO ULIOTOLEWA NA MAREHEMU EDDINGTON KISASI

    Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Serikali inathamini michango uliotolewa na aliekuwa  Kamishna wa   Kwanza wa Polisi Zanzibar Marehemu  Eddington Herbert Kisasi  katika harakati  Mapinduzi ya Zanzibar na baada ya Mapindunzi.

WANANCHI KUWAENZI VIONGOZI WALIOITUMIAKIA NCHINI

    Wananchi Wilaya ya Kusini wametakiwa kuwaenzi Viongozi walioitumiakia Nchini na kuleta maendeleo katika Serikali.

     Hayo yameelezwa na Mhe.Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano  Mhe.Nadir Abdul-latif katika Dua maalum ya kumuombea Raisi wa Awamu ya Nne Sheikh Idrissa Abduli Wakili katika Kaburi lake liopo Kiongoni.

     Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawajibu wa kuwaombea Dua Viongozi hao kila ifikapo Mwezi wa Nne wa kila Mwaka ambapo ni utaratibu wao waliojiwekea kama ni sehemu ya kuwaenzi.

FIKRA NA FALSAFA ZA MAREHEMU KARUME KUENDELEZWA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussen Ali Mwinyi amewataka Wananchi kuzienzi na kuziendeleza  fikra na falsafa za kimaendeleo na kizalendo za Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwa maslahi ya Taifa.

RAIS SAMIA AMEAGIZA KUSAJILIWA TAASISI ZOTE ZA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA WATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka tume ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Tanzania (PDPC) kuhakikisha ifikapo Disemba Mwaka huu iwe imezisajili Taasisi zote za Umma na Binafsi zinazohusika na ukusanyaji na uchakataji wa Taarifa na kuzisimamia kwenye kutekeleza sheria ya ulinzi wa Taarifa Binafsi. 

ZSSF IMETAKIWA KUTUNZA VIELEZO VYA MATUMIZI YA FEDHA

Kamati ya kuchunguza na kudhibiti Hesabu za Serikali (PAC) ya Baraza la Wawakilishi imesisitiza Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kutunza na kuhifadhi vielezo vya matumizi ya fedha za Serikali ili kuepusha kuibuka kwa hoja za CAG.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Juma Ali Khatibu amesema hayo baada ya kupata majibu ya hoja za Ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa Hesabu za Mashirika na Taasisi za Serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwa Mwaka wa Fedha unaoishia 2022.

WATENDAJI WA TASAF WAMEHIMIZWA KUSIMAMIA VIZURI MIRADI

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imesisitiza kusimamiwa vizuri Miradi inayotekelezwa katika Mpango wa kunusuru kaya Masikini Tasaf ili iweze kufikia tija iliyokusudiwa.

Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mwanaasha Khamis Juma wametoa ushauri katika ziara ya kukagua Miradi ya Tasaf iliyotekelezwa Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na kupokea Taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya Masikini kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024.

TRC IMEPOKEA KICHWA CHA KWANZA CHA TRENI CHENYE MUUNDO WA MCHOMOKO

Shirika la Reli Tanzania TRC limepokea Kichwa cha kwanza cha Treni chenye Muundo wa mchomoko na uwezo wa kuunganisha Mabehewa nane yenye uwezo wa kubeba abiria Mia Tano na Themanini na Tisa kwa wakati Mmoja.

Akizungumza katika Hafla ya ushushaji Bandarini Jijini Dar-Es-Salaam, Waziri wa uchuzi Mhe Profesa Makame Mbarawa amesema, Kichwa kilichopokelewa ni Miongoni mwa Vichwa Kumi vinavyotengenezwa na Kampuni ya Huindai Rotam ya Nchini Korea ya Kusini.

SMZ INATHAMINI MCHANGO WA MAREHEMU THABIT KOMBO

Waziri wa  Utalii na Mambo ya Kale  Mhe Mudrik Ramadhan Soraga  ameungana na Wananchi katika  Dua ya kumuombea aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa chama cha Afro  Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo  huko Chukwani .

Akizungumza mara baada ya Dua hiyo Waziri Soraga amesema  Serikali inathamini mchango uliotolewa na Kiongozi huyo katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar na kipindi chote cha Uongozi wake 

TAASISI ZA FEDHA NCHINI ZATAKIWA KUWEZESHA MAWAKALA

    Taasisi za Fedha Nchini zimetakiwa kuwawezesha Mawakala kwa kuwapatia Mikopo kwa muda sahihii pale inapohitajika kwa lengo la kuwahudumia Wananchi na kukuza uchumi wa Nchi.

    Akizungumza baada Iftari iliyoandaliwa na Kampuni ya Said Holding huko Mlandege Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh:Ayoub Moh'd Mahmoud amesema hatua hiyo itawezesha Mawakala kukuza uchumi wao  na kulipa Kodi kwa wakati 

WANAWAKE WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUANZISHA BIASHARA

    Zaidi ya Wanawake 300 wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Wamepatiwa mbinu za kuanzisha Biashara ili kukuza Uchumi wao na kuondokana na tatizo la kuwa Tegemezi kwa kutambua fursa zilizopo.

    Akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake la Chanuo Sumiti Meneja Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa Jambo Group Nickson George,amesema wamelenga kukuza Uwekezaji kwa kutumia fursa zilizopo kikiwemo Kilimo,Ufugaji wa Samaki na Madini.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.