WANAWAKE WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUANZISHA BIASHARA

Kongamano Wanawake

    Zaidi ya Wanawake 300 wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Wamepatiwa mbinu za kuanzisha Biashara ili kukuza Uchumi wao na kuondokana na tatizo la kuwa Tegemezi kwa kutambua fursa zilizopo.

    Akizungumza kwenye Kongamano la Wanawake la Chanuo Sumiti Meneja Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa Jambo Group Nickson George,amesema wamelenga kukuza Uwekezaji kwa kutumia fursa zilizopo kikiwemo Kilimo,Ufugaji wa Samaki na Madini.

    Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo Mkoa wa Shinyanga Jonathan Kifunda,amesema bado kuna fursa nyingi ambazo Wafanya biashara hawajazitumia kukuza uchumi wao.

    Nao baadhi ya Wanawake  wakazungumzia umuhimu wa Kongamano hilo katika kutumia fursa za Biashara.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.