Habari

WANAFUNZI MPENDAE WATAKIWA KUSOMA KWA MALENGO

    Mbunge wa  Jimbo la Mpendae Mhe.Taufiki Salum Turki amewakumbusha  Wanafunzi wa Skuli ya Mpendae kusoma kwa  malengo ili waje kuwa Viongozi wa baadae.

    Akizungumza katika  Hafla  kutoa Chakula na Projector kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita wa Skuli ya Mpendae amesema  kuyatambua malengo yao kutamuwezesha Mwanafunzi kujitambua.   

ZAWA YAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UKOSEFU WA MAJI NCHINI

     Mamlaka ya Maji Zanzibar 'ZAWA' imehimizwa kuchukua hatua madhubuti  zitakayowawezesha Wananchi wa maeneo ya Mjini na Vijijini kupata huduma za Maji Safi Salama.

     Wajumbe wa Kamati ya Ardhi Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Yahya Rashid Abdallah wametoa mapendekezo hayo mara baaada ya kutembelea na kupokea Taarifa ya utekekelezaji wa mradi wa kulaza mabomba Unguja na Pemba.

KAMATI PAC YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA IPA

     Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe.Machano Othman Said ameutaka Uongozi wa Chuo cha Utawala wa Umma kuanza hatua za Awali za Ujenzi wa Tawi Jipya Kisiwani Pemba.

    Mhe.Machano Akizungumza katika Kikao cha kupokea Taarifa ya Chuo hicho kwa Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 amesema hatua hiyo itasaidia kuondosha tatizo liliopo hivi sasa la ukosefu wa Eneo la kudumu ambao limekuwa halikidhi mahitaji na ubora katika ufundishaji.

SMZ YAENDELEA KUYAENZI MATUNDA YA MAPINDUZI

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kukumbuka vyema matunda yatokanayo ya Waasisi wa Mapinduzi katika kujenga Maendeleo ya Wazanzibari.

    Akizungumza Katika Dua Maalumu ya kuwaombea Viongozi Waasisi wa Taifa katika Kaburi la Marehemu Said Washoto Mnyuke huko Mndo Wilaya ya Magharib 'a' Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe Nadir Abdullatif Yussuf amesema Viongozi hao wameacha athari kubwa katika maendeleo ya Wazanzibar hivyo nilazima kuzienzi juhudi zao na kuwaombea Dua ili kupata Rehma za Mwenyezi Mungu

SERIKALI YAENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuepuka matumizi ya Dawa za Kulevya kwani yanaharibu nguvu kazi ya Taifa hasa Vijana ambao wanategemewa kuongoza na kufanya shughuli za uzailishaji pamoja na kuharakisha maendeleo.

     Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli katika Sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zilizofanyika kitaifa katika Uwaja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE 2024 YAMEKAMILIKA

Waziri wa Habari, Vijana na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tabia Maulid Mwita amesema Maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 yamekamilika huku akiwataka Watanzania kushiriki katika Uzinduzi huo.

Waziri Tabia amatoa Kauli hiyo akiwa katika Uwanja wa Chuo cha ushiriki Moshi Mkoani Kilimanjaro Mara baada ya kukagua Maandalizi ambapo amesema Waziri Mkuu Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.

VIONGOZI WASISITIZA KUFANYA MEMA ILI KUKUMBUKWA BAADAE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Ali Suleiman Ameir amewasisitiza Viongozi kutumia hekima, Busara na kufanya Matendo Mema ili kuwa kigezo na kukumbukwa hapo baadae.

Akizungumza katika Ziara ya kumuombea Dua aliyekuwa Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdallah Said Natepe iliyofanyika Kijijini kwao Mwache ALale Wilaya ya Magharibi “A” amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha uzalendo kwa Wananachi.

Aidha amesema ni vyema kuendelea kuwakumbuka kwa kuwaombea dua Viongozi hao ili kukumbuka uzalendo na hekima walizokuwa nazo katika kulituumikia Taifa.

WANANCHI WA DONGE WAMETAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MAJI

Wananchi wa Donge Meli Ishirini wametakiwa kutunza Miundombinu ya Maji safi na salama inayowekwa na Serikali pamoja na Wadhamini mbalimbali katika maeneo yao.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed  ameeleza hayo wakati akizinduwa Kisima cha Maji safi na salama kilichochimbwa na wafadhili legasy aid group Foundation katika eneo la Donge Meli Ishirini.

Dk. Khalid amewanasihi Wananchi hao kuthamini juhudi hizo kwa kutunza Miundombinu hiyo ikiwemo Mfumo wa matumizi ya Nishati ya Juwa inayotumika katika uendeshaji wa Kisima hicho.

WAZIRI MKUYA KUIMARISHA MFUMO WA HUDUMA ZA PENCHENI JAMII KWA WAZEE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Fedha na Mipango  Mh Sada Mkuya Salum amesema  wataendelea kuimarisha Mfumo wa  huduma za Pencheni  Jamii kwa Wazee kupitia Mifumo  ya Kidigitali ya kuwasajili na Account za  Bank ya PBZ ili kuepukana  na matatizo yanayojitokeza.

WATUMISHI WA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU KUFANYAKAZI KWA UADILIFU.

Wafanya kazi wa Mdhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali Kisiwani Pemba  wameshauriwa  kufanyakazi kwa Mujibu  wa Mkataba wa uwajiri wao  ili kuepuka  matatizo  kwa Jamii na kwa MwenyeziMungu .

Ushaur huo umetolewa na  Mratibu wa Ofisi ya Mufti Pemba Nd.said Ahmad Mohamed  wakati alipokuwa akizungunza na Watendaji wa Taasisi  hiyo huko katika Ukumbi wa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba  ,katika hafla ya kuwaombea Dua waliokua Watumishi wa Taasisi  hiyo pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali 

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.