VIONGOZI WASISITIZA KUFANYA MEMA ILI KUKUMBUKWA BAADAE

MHE. ALI SULEIMAN AMEIR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Ali Suleiman Ameir amewasisitiza Viongozi kutumia hekima, Busara na kufanya Matendo Mema ili kuwa kigezo na kukumbukwa hapo baadae.

Akizungumza katika Ziara ya kumuombea Dua aliyekuwa Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdallah Said Natepe iliyofanyika Kijijini kwao Mwache ALale Wilaya ya Magharibi “A” amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha uzalendo kwa Wananachi.

Aidha amesema ni vyema kuendelea kuwakumbuka kwa kuwaombea dua Viongozi hao ili kukumbuka uzalendo na hekima walizokuwa nazo katika kulituumikia Taifa.

Nae Mtoto wa Marehemu Said Natepe Ali Abdallah Natepe  kwa Niaba ya Familia amesema wamefarajika kwa kuona Mzee wao bado anathaminiwa kutokana na mchango alioutoa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.