KAMATI PAC YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA IPA

Kamati BLW

     Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe.Machano Othman Said ameutaka Uongozi wa Chuo cha Utawala wa Umma kuanza hatua za Awali za Ujenzi wa Tawi Jipya Kisiwani Pemba.

    Mhe.Machano Akizungumza katika Kikao cha kupokea Taarifa ya Chuo hicho kwa Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 amesema hatua hiyo itasaidia kuondosha tatizo liliopo hivi sasa la ukosefu wa Eneo la kudumu ambao limekuwa halikidhi mahitaji na ubora katika ufundishaji.

     Wakichangia Taarifa hiyo Wajumbe wa Kamati hiyo  wamesema wameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa Majukumu ya Chuo. 

     Akitoa Taarifa fupi  kwa Kamati hiyo kwa Robo ya Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Mkuu wa Chuo cha Utawala wa Umma IPA Dk.Shaaban Mwinchum Suleiman amesema Chuo kimefanikiwa   kutayarisha Mapitio ya Kanuni na Miongozo  inayosaidia uendeshaji wa shughuli za Chuo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.