SMZ YAENDELEA KUYAENZI MATUNDA YA MAPINDUZI

DUA YA KUMUOMBEA MUASISI WA MAPINDUZI

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kukumbuka vyema matunda yatokanayo ya Waasisi wa Mapinduzi katika kujenga Maendeleo ya Wazanzibari.

    Akizungumza Katika Dua Maalumu ya kuwaombea Viongozi Waasisi wa Taifa katika Kaburi la Marehemu Said Washoto Mnyuke huko Mndo Wilaya ya Magharib 'a' Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe Nadir Abdullatif Yussuf amesema Viongozi hao wameacha athari kubwa katika maendeleo ya Wazanzibar hivyo nilazima kuzienzi juhudi zao na kuwaombea Dua ili kupata Rehma za Mwenyezi Mungu

    Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Familia Mfaume Said Washoto amesema Wanaishukuru Serikali kwa kuanisha utaratibu wa kuwaombea Dua Viongozi hao jambo ambalo linawapa Faraja Familia zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.