WANANCHI WA DONGE WAMETAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MAJI

DKT. KHALID SALUM MOHAMMED

Wananchi wa Donge Meli Ishirini wametakiwa kutunza Miundombinu ya Maji safi na salama inayowekwa na Serikali pamoja na Wadhamini mbalimbali katika maeneo yao.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed  ameeleza hayo wakati akizinduwa Kisima cha Maji safi na salama kilichochimbwa na wafadhili legasy aid group Foundation katika eneo la Donge Meli Ishirini.

Dk. Khalid amewanasihi Wananchi hao kuthamini juhudi hizo kwa kutunza Miundombinu hiyo ikiwemo Mfumo wa matumizi ya Nishati ya Juwa inayotumika katika uendeshaji wa Kisima hicho.

Msimamizi wa Legasy Aid Group Foundation amesema Kisima hicho kimejengwa katika matumizi ya Sola hatua ambayo ni itawasaidia Wananchi kutolipia gharama za Umeme. 

Wananchi wameishukuru Serikali   na Wafadhili hao kwa kuwatatulia matatizo mbalimbali yanayowakabili yakiwemo Maji .

Wafadhili hao wanatarajia kujenga Visima hivyo  sehemu mbalimbali za Unguja na Pemba

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.