Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mh Sada Mkuya Salum amesema wataendelea kuimarisha Mfumo wa huduma za Pencheni Jamii kwa Wazee kupitia Mifumo ya Kidigitali ya kuwasajili na Account za Bank ya PBZ ili kuepukana na matatizo yanayojitokeza.
Akizungumza na Wazee na Masheha katika Mkutano wa wanufaika wa Pencheni Jamii na Afisi ya Raisi Fedha na Mipango katika Ukumbi wa Baraza la Wakilishi la zamani amesema lengo ni kuona Wazee wanasajiliwa kwa kupatiwa Account Bank za PBZ ili kuwaingizia Fedha zao za Pencheni.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema wataendelea kupokea matatizo yanayowapata Wazee na kuyafanyia kazi ili wapate haki zao za msingi zinazostahiki
Kaimu Mkurugenzi kutoka Benki ya PBZ Anwar Abdallah Salehe amesema malengo yao ni kuwawezesha Wazee kuwafungulia Account ambazo zitawasaidia kupokea Penchani zao kwa uhakika na urahisi
Wazee wanaopokeya Pencheni wametowa Shukrani zao kwa Benki hiyo kwa kuwapatia usajili huo na kuwaomba Wazee wenzao kuwenda kwa Masheha wao ili na wao wasajiliwe ili wapate haki zao