WAZIRI MKUYA KUIMARISHA MFUMO WA HUDUMA ZA PENCHENI JAMII KWA WAZEE

MHE.SADA MKUYA SALUM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Fedha na Mipango  Mh Sada Mkuya Salum amesema  wataendelea kuimarisha Mfumo wa  huduma za Pencheni  Jamii kwa Wazee kupitia Mifumo  ya Kidigitali ya kuwasajili na Account za  Bank ya PBZ ili kuepukana  na matatizo yanayojitokeza.

Akizungumza na Wazee na Masheha katika Mkutano   wa wanufaika  wa Pencheni Jamii na Afisi ya Raisi Fedha  na Mipango katika Ukumbi wa Baraza la Wakilishi la zamani  amesema   lengo ni kuona  Wazee wanasajiliwa  kwa kupatiwa  Account Bank za PBZ ili kuwaingizia Fedha zao za  Pencheni.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia  Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema wataendelea  kupokea matatizo  yanayowapata Wazee na kuyafanyia  kazi ili  wapate haki zao za msingi zinazostahiki

Kaimu Mkurugenzi kutoka Benki  ya PBZ Anwar Abdallah Salehe amesema malengo  yao ni kuwawezesha Wazee  kuwafungulia Account   ambazo zitawasaidia   kupokea  Penchani zao kwa uhakika na urahisi   

Wazee wanaopokeya  Pencheni wametowa Shukrani zao    kwa Benki  hiyo kwa kuwapatia   usajili  huo na kuwaomba Wazee wenzao kuwenda kwa Masheha wao ili na wao wasajiliwe ili wapate haki zao

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.