Habari

ZRA YAPELEKA FARAJA KWA WATU WENYE MAZINGIRA MAGUMU

    Mamalaka ya Mapato Zanzibar ZRA, imesema itaendelea kusaidia Watu wenye mazingira magumu na wenye Ulemavu ili kujiona wanathamani ndani ya Jamii.

     Akizungumza mara baada ya kugawa sadaka kwa Familia 300 ikiwemo Watu wenye mazingira magumu, Watoto wenye Ulemavu na Watu wasiojiweza, huko Bumbwini na Jangombe,  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamalaka hiyo, Profesa Hemed Rashid Hikman.

WAKRISTO ZANZIBAR WASHEREHEKEA PASAKA KWA AMANI NA UTULIVU

    Waumini wa Dini ya Kikiristo wametakiwa kusherehekea Skukuu ya Pasaka kwa Amani na Utuli bila kuathiri Jamii.

     Hayo yameelezwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la ZICC Karikoo Zanzibar Bishop Dickson Kaganga katika  kusherehekea Skukuu ya Pasaka amesema ni vyema kwa Waumini wa Dini ya Kikiristo Kumcha Mungu kwa   kuheshimu Dini ya Kiislam hasa katika  mfungo  huu wa Ramadhan.

WAISLAMU WANAWAKE WAMETAKIWA KUSIMAMIA MISINGI YA QUR’AN

    Wanawake wa Kiislam wametakiwa kuendelea Kuihifadhi Qur-an na kusimamia misingi yake ili kuweza kuleta mabadiliko katika malezi ya Familia zao .

     Katibu  Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Mhandisi Zena Ahemed Said ametoa ushauri huo katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Kina Mama Watu Wazima na kuwataka Kusoma Qur-an na kuielewa ili kuacha makatazo  yake na misingi bora kwa Jamii kwa kuzingatia Wanawake ndio Walezi wa Familia. 

MAMIA YA WATU WAJITOKEZA KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN ZANZIBAR

    Kijana Mahmoud Kassim kutoka Zanzibar Mwenye Umri wa Miaka 20 ameibuka Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Afrika Mashariki na kuzawadiwa Fedha Taslim sShiling Milioni Thelathini za Kitanzania.

DKT.MWINYI AWAHIMIZA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUSOMA QURANI TUKUFU

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea kusoma Qurani Tukufu  na kufuata maelekezo yake ili Jamii iweze kufanikiwa Duniani na Akhera.

     Dk.mwinyi ametoa wito huo katika kilele cha tunzo za Kimataifa za  Qur-an Tukufu zilizoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhisha  Qur-ani  Tanzania chini ya Uongozi wa Sheikh Othman Kaporo na kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Diamond Jubilee

SERIKALI KUKABILIANA NA HALI YA UGUMU WA MAISHA KWA WANANCHI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itachukua jitihada za kukabiliana na hali ya ugumu wa maisha kwa kadri ya hali itakavyoruhusu ili kuwapunguzia mzigo Wananchi.

   Akizungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi katika Ikulu ya Pagali, amesma kupanda kwa gharama za maisha kunachangiwa na matatizo katika uchumi wa Dunia zikiwemo, vita, kupanda bei kwa bidhaa za nje na baadhi ya Mataifa Duniani kuzuia kuuza bidhaa zao kwa Mataifa mengine.

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI YA CAG NA TAKUKURU DODOMA

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa Mwaka 2022/2023.

     Akizungumza mara baada ya kupokea Taarifa hiyo Rais Samia amesema kuwa ripoti hizo zinazosomwa kila Mwaka zinachangia maboresho katika kuimarisha utendaji kazi kwa Serikali pamoja na Mashirika ya Umma.

SMZ KUIMARISHA MAZINGIRA RAFIKI YA UCHUMI

Serikali itaendelea kuweka Mazingira Rafiki na wezeshi ya kiuchumi ili kukuza sekta ya Fedha Nchini.

Katika uzinduzi wa Ripoti ya utafiti Finscope Tanzania 2023 kwa upande wa Zanzibar, uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ametaja miongozni mwa mikakati hiyo ni kuunda sera zinazozingatia mahitaji ya Sekta ya fedha.

VIKOSI VYA SMZ VIJENGEWE UWEZO KUIMARISHA UZALISHAJI

Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, imeiomba Serikali kuendelea kuvijengea uwezo Vikosi vya Idara Maalum za SMZ, ili viweze kuimarisha uzalishaji wa Kilimo na ufugaji. 

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, Mh Machano Othman Said, akizungumza baada ya kutembelea Vikosi vya Idara Maalum, amesema wamebaini kuwa vikosi hivyo vinaendesha Miradi yake ya uzalishaji bila ya kuwa na Utaalamu wa kutosha na kupelekea kushindwa kujitegemea.

BILIONI 13 KUIMARISHA MIUNDOMBINU HOSPITAL YA MARA

Jumla ya Shilingi Bilion 13 zimetolewa na Serikali katika kuongeza Miondombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere iliyopo Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Wodi mpya ya kisasa ya Watoto.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kukagua Miundombinu iliyopo ambapo alibainisha Fedha hizo zilizotolewa na Serikali katika kuimarisha Miundombinu ya Majengo, Umeme na Wodi ya Watoto Wachanga.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.