Kijana Mahmoud Kassim kutoka Zanzibar Mwenye Umri wa Miaka 20 ameibuka Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Afrika Mashariki na kuzawadiwa Fedha Taslim sShiling Milioni Thelathini za Kitanzania.
Akizungumza baada ya Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar kwa kushirikiana na Ofisi ya Muft Mkuu na kuhusisha Mataifa Manane Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haj Hussein Ali Mwinyi amesema Vijana ndio nguvu kazi ya Baadae na nyenzo ya maadili katika Jamii hivyo Waalimu wa Madrasa na Wazazi waendelee kuweka juhudi za makusudi katika kukuza Maadili ya Vijana
Aidha Alhaj Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuunga Mkono mambo ya kheri katika Nchi na kufahamisha kuwa Mashindano ya Quran Zanzibar yatakuwa endelevu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ndg.Ramadhan Bukini na Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Shekh Khalid Mfaume wamesema lengo la Mashindano hayo ni kuwaunganisha Wazanzibar kuwa kitu kimoja huku wakitoa shukran kwa Mashirikiano waliyoyapata kutoka kwa Viongozi wa Taasisi mbalimbali Nchini.
Mashindano hayo yamehusisha Nchi ya Tanzania ,Comoro, Kenya Burundi Uganda Rwanda na Wenyeji Zanzibar ambapo Nafasi ya Pili imechukuliwa na Comoro na Fedha Milioni 20 huku nafasi ya Tatu ikishikiliwa na Kijana Abdurahmaan Mussa Miaka 14 kutoka Kenya na amepata Shilingi Milioni 10 .