Habari

ZAIDI YA VITABU 600 VYA KISWAHILI VIMETOLEWA NA ALAF KUKUZA FASIHI

Zaidi ya Vitabu 600 zimetolewa kwa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Bodi ya huduma za Maktaba Zanzibar na Baraza la Kiswahili la Zanziba na Kampuni ya ALAF LTD ambao ni Wachapishaji wa Vitabu hivyo ili kukuza fasihi na kujenga utamaduni wa kusoma Vitabu.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa Machapisho ya Kiswahili, Afisa uhusiano wa Alaf Tanzania, Thuresia Mmasy, amesema Taasisi inatambua thamani ya Lugha ya Kiswahili na kuamini kuwa Taasisi zilizopatiwa Vitabu zina mchango katika kuendeleza masomo ya Kitaaluma na utafiti wa kiswahili.

PROF. MBARAWA AMEONGOZA MAJARIBIO YA MELI YA MV MWANZA

Waziri wa uchukuzi profesa Makame Mbarawa ameongoza Zoezi la Safari ya majaribio ya Meli ya Mv. Mwanza hapa kazi tu ambayo Ujenzi wake umefikia asilimia 96.

Meli hiyo imeng’oa Nanga majira ya Mchana katika Bandari ya Mwanza kusini chini ya Uongozi wa Nahodha Bembele Ng’wita

Waziri Profesa Mbarawa akizungumza baada ya kushuhudia jaribio la Meli hiyo amesema zoezi hilo limefanyika kwa ufanisi mkubwa.

Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Meja Jenerali Paul Simuli ametoa Rai kwa Wafanyabiashara kuitumia Meli hiyo katika shughuli za Kibiashara.

WANANCHI WAMEOMBA KUHARAKISHWA UJENZI WA MITARO

Wakaazi wa Mpendae wameelezea wasiwasi wao wa kukamilika mitaro kwa wakati hasa katika kipindi hiki cha Mvua hali inayoweza kuathiri Makaazi yao.

Katika ziara zinazoendelea kufanywa na Mfuko wa Barabara Zanzibar UUB, Wakaazi hao wamesema Mvua zinazoendelea kunyesha zinaweza kuathiri hivyo wameziomba Mamlaka husika kuhakikisha Mitaro inakamilika kwa wakati.

Akitolea ufafanuzi malalamiko ya Wananchi, Mhandisi Hassan Ameir Hassan kutoka Mfuko wa Barabara amewatoa shaka Wananchi na Ujenzi unaenda kwa haraka ili kupeuka usumbufu katika kipindi hiki.

WATU 28 WANASHIKILIWA NA POLISI MOROGORO KWA TUHUMA ZA UPORAJI

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 28 pamoja na Pikipiki 29 ambazo zilikuwa zikitumiwa na watuhumiwa hao kwenye uporaji wa Simu na Vitu vingine kutoka kwa Wananchi Manispaa ya Morogoro.

Kuwepo kwa Waporaji kwa njia ya Pikipiki kuliibua sintofamu kwa Wakazi Manispaa ya Morogoro ambapo kutokana na tatizo hilo Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Morogoro Sacp Alex Mkama amesema tangu Mwezi Januari hadi Machi Mwaka huu wamefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa wa uporaji pamoja na uporaji.

WEMA NA SEMUKA YATILIANA SAINI UCHAPISHAJI VITABU

    Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Amali imetiliana Saini  na Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Semuka Mkataba wa Uchapishaji wa Vitabu kwa ajili ya Skuli za Binafsi Zanzibar.

  Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Ali Abdulgulam Hussein  amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wake wanapata Elimu iliyobora hivyo inachukua juhudi mbalimbali kuimarisha miundombinu ya Elimu.

ZMUX YAKABIDHIWA MUUNDO WA KUIMARISHA UFANISI WA KAZI

    Katibu wa  Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Kubingwa Mashaka Simba  amekabidhi muundo wa Taasisi ya  Kampuni ya Uunganishaji  na Usambazaji Maudhui Zanzibar ZMUX  ili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi .

    Akikabidhi muundo huo  huko  Mwanakwerekwe  Kubingwa amesema ni vyema Muundo huo  kutekeleza maelekezo yake ili kuleta ufanisi katika kazi na kila Mtendaji akapangiwa Majukumu yake .

MV MWANZA HAPA KAZI TU ; YAANZA SAFARI YA KWANZA YA MAJARIBIO YA KIUFUNDI ZIWA VICTORIA

     Meli Mpya ya kubeba Abiria na Mizigo ya MV Mwanza hapa kazi tu, kwa mara ya kwanza imeanza safari ya kwanza ya majaribio ya kiufundi katika Ziwa Victoria.

     Meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa ni Watu 60, wakiwemo Wahandisi, Wakandarasi na Wataalam waliokuwa wakiijenga.

     Meneja Mradi wa Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu Vitus Mapunda amesema majaribio hayo ni ishara ya kukamilika kwa Ujenzi wa Meli hiyo.

HUDUMA YA TIGO BIMA HURAHISISHA MAISHA YA WATANZANIA

     Waziri wa Fedha na Mipango Drk.Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu wa Tigo Zantel kuhakikisha huduma ya Tigo Bima inaendana na Wananchi  kwa  kuwa na tija na Serikali.

     Akizindua huduma mpya  ya Tigo Bima kwa  Vyombo ya Moto huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege  amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza Mapato ya Serikali na kuongeza  Uchumi wa Nchi kwa njia ya Kidigitali.

VIWANDA VYA IDARA MAALUM ZA SMZ KUCHOCHEA FURSA ZA AJIRA NCHINI

    Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeridhishwa na maendeleo ya Viwanda vya Idara Maalum za SMZ na kueleza kwamba uwekezaji huo utachochea  upatikanaji wa Ajira pamoja na kuondokana na uagizaji wa vitu visivyo na ubora Nje ya Nchi.

    Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Machano Othman Said wametoa rai hiyo wakati walipotembelea Kiwanda cha Ushoni wa bidhaa mbali mbali ikiwemo Nguo, Viatu, Uchapaji na Uzalishaji wa mifuko kinachosimamiwa na Idara Maalum za SMZ.

MAJAALIWA AONGOZA WANANCHI MAPOKEZI YA NDEGE BOEING 737-9MAX

     Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amewataka Wafanya kazi wa Shirika la Ndege Tanzania ATCL kufanyakazi kwa uzalendo pamoja na kufanya tafiti za miruko ya Ndege ya ATCL ili kuweza kuleta tija na kuepuka kubadili ratiba za mara kwa mara za safari za Ndege za Shirika hilo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.