ZAIDI YA VITABU 600 VYA KISWAHILI VIMETOLEWA NA ALAF KUKUZA FASIHI

CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR SUZA

Zaidi ya Vitabu 600 zimetolewa kwa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Bodi ya huduma za Maktaba Zanzibar na Baraza la Kiswahili la Zanziba na Kampuni ya ALAF LTD ambao ni Wachapishaji wa Vitabu hivyo ili kukuza fasihi na kujenga utamaduni wa kusoma Vitabu.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa Machapisho ya Kiswahili, Afisa uhusiano wa Alaf Tanzania, Thuresia Mmasy, amesema Taasisi inatambua thamani ya Lugha ya Kiswahili na kuamini kuwa Taasisi zilizopatiwa Vitabu zina mchango katika kuendeleza masomo ya Kitaaluma na utafiti wa kiswahili.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa Suza mipango Fedha na Utawala, Dkt. Hashim Hamza Chande, amewataka Waandishi wa Vitabu kuendeleza Fani yao ili kukuza ujuzi wa Fasihi na kuendelea kuwa Waandishi wazuri hapo baadae.

Mkurugenzi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Mohamed Khamis Kombo na Wadau wa Kiswahili wamewasisitiza Waandishi kuendelea kutunga Vitabu ili kuendeleza kiswahili.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.