Habari

WANAWAKE KISIWANI PEMBA WASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA DKT.SAMIA

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amewashukuru Wanawake wa Zanzibar kwa mashirikiano yao katika kumjali na kumuombea Dua ambayo kwake ni zawadi kubwa inayompa faraja.

     Dr. Samia ametoa shukran hizo huko katika Ukumbi wa Viwanja vya kufurahishia Watoto Tibirinzi Chake Chake wakati alipokuwa akizungumza na Wanawake katika Dua maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake.

WAZAZI WASISITIZWA KUSIMAMIA WATOTO WAO ILI WAWE NA MAADILI MEMA

Wazazi wamesisitizwa kuwasimamia Watoto wao kupata msingi mzuri wa Elimu ya Dini ili waweze kuwa na maadili mema na Viongozi waadilifu wa baadae.

Akizungumza katika Mashindano Makuu ya Kuhifadhi Qur an Zoni ya Fuoni Meli Sita Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni Yussuf Hassan Iddi amesema watoto ni hazina ambayo inahitaji kusimamiwa kujifunza mambo ya Kheri yatayowasaidia kukiendeleza Kizazi hicho

Aidha amesema hivi sasa suala la uaminifu limepungua katika Jamii hivyo ni muhimu Watoto wakuzwe katika miongozo ya kuwajenga kuwa Waaminifu 

WAZIRI TABIA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Tabia Maulid Mwita, amefanya ziara ya kustukia  katika Ofisi za Baraza la Michezo na Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni na kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyakazi wa Taasisi hizo.

Hayo yamejiri huko Baraza la Michezo Mwanakwerekwe, Ambapo Waziri Tabia baada ya kupokea malalamiko hayo amewataka Viongozi wa Taasisi hizo kuyatatua mara moja huku akisisitiza uwajibikaji katika kwa lengo la kupatikana ufanisi.

MAFANIKIO SHIRIKA LA RELI TANZANIA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

Shirika la Reli Tanzania  TRC limesema katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Shirika hilo limefanikisha kujenga Kilomita 1,560 za Mradi wa Reli ya kisasa  ya SGR.

Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  hilo  Masanja Kadogosa  amesema Thamani ya uwekezaji wa Mradi huo imefikia Trioni 23.3ukiondoa kipande cha Uvinza hadi Musongati ambapo kipo katika  hatua ya ununuzi ambapo kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Trioni 10.01 zimeshalipwa kwa Wakandarasi .

SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR IMEZINGATIA MASLAHI YA WANANCHI

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dtk. Emmanuel John Nchimbi amesema uamuzi wa kuwepo kwa Serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar ulizingatia usalama wa maisha ya Watu kuliko maslahi ya Vyama vya Siasa.

Dkt. Nchimbi amesema kuwepo Serikali ya umoja wa Kitaifa umeondoa hali ya Siasa za Chuki na Uhasama, huku akisisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kuongoza kwa misingi ya haki na uwajibikaji ili kudumisha umoja na utulivu Nchini.

WEMA IMEWATAKA WAHITIMU KIDATO CHA SITA KUTUMIA FURSA WALIZOZIPATA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Wahitimu  Waliofaulu Kidatu cha Sita  kutumia vyema fursa walizozipata za kuendelea na Masomo ya Elimu ya juu  ili kutimiza malengo  yao na ya  Serikali ya kuzalisha Wataalamu mahiri.

DKT. NCHINIMBI AELEZEA MCHANGO WA WAZEE KATIKA MAENDELEO

    Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema maendeleo yaliyofikiwa Nchini yametokana na juhudi kubwa za kiutendaji zilizoasisiwa na Wazee wa Chama hicho waliohudumu kwa bidii na maarifa katika sekta za Umma na Binafsi.

    Kauli hiyo imeitoa katika Ziara yake Siku Moja Kisiwani Pemba Wakati kujitambulisha na kuzungumza na Mabaraza ya Wazee wa CCM wa Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba huko Ukumbi wa Makonyo Wilaya ya Chake Chake.

BODI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

     Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya uimarishaji wa miondombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume.

    Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa Viwanja vya Ndege, Ndg.Laila Burhan Ngozi amesema hayo wakati wa Ziara maalum ya kukagua miradi ya uimarishaji wa miundombinu katika Uwanja vya Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume.

     Amesema utekelezaji wa miradi hiyo unaridhisha kwa Asilimia kubwa licha ya kuwa imeanza kwa muda mfupi.

VIONGOZI WATOA MSAADA WA UJENZI WA MADRASA YA MPENDAE

    Viongozi wa Jimbo la Mpendae  akiwemo Muakilishi Mhe.Shaabani Ali Muhammed  na Mbunge Ndg.Taufiki Salum Turkii  wamewataka Waislamu kutoa katika mambo ya kheri ili kupata radhi kwa mola wao .

    Wakizungumza katika hafla ya kukabidhi  mifuko ya Saruji miatatu kwa ajili ya Madrasa akiwa  huko katika Mskitini wa kwa Ameir Tajo wa Mpendae wamesema jambo hilo huleta mapenzi baina Watu Wa chini na wenye uwezo.

SHILINGI BILIONI 190.6 ZATUMIKA KUBORESHA MIRADI RUKWA
Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.