Habari

TARURA YABAINI MADARAJA 19 YAMESOMBWA NA MVUA RUVUMA

     Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoani Ruvuma imebaini Jumla ya Madaraja 19 ambayo yamesombwa na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani hapo katika Ripoti iliyosomwa kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo mtela Mwampamba.

KOICA YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SMZ KATIKA KUKUZA MAENDELEO

    Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar itaendelea kushirikiana na Mashirika mbali mbali ya Kimataifa, ili kuhakikisha inaongeza ufaulu wa Masomo ya Sayansi na kuondosha Zero katika Mitihani ya Taifa.

DKT.MWINYI AWASISITIZA WAISLAMU KUHIFADHI QUR-AN

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuhifadhi Qur-an Tukufu na kufundisha Wwatoto wao pamoja na kutoa Sadaka kwa Watu wenye mahitaji.

ZRA WAWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUATA SHERIA

    Wafanyabiashara wanaosafirisha na kuingiza mizigo Zanzibar kutoka Nje ya Nchi wameshauriwa  kufanya Biashara hiyo kwa kuzingatia sheria

    Akikagua Wafanyabiashara wanauza Biashara zao kwa kuingiza  kutoka Nje Kamishna Mkuu ZRA Ndg. Yussuf Juma Mwenda amesema kumekuwa na taratibu za sheria zinakiukwa na baadhi ya Wafanyabiashara kupata hasara kwa kukosa kutoa malalamiko yao wakati wa marejesho ZRA.

UBORA WA QUR-AN NI MUHIMU DUNIANI NA KESHO AKHERA.

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Hussein Ali Mwinyi amesema ubora wa Quran ni muhimu katika maisha ya Duniani na kesho Akhera.

    Akizungumza katika Fainali ya Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Quran Tajweed Alhajj Mwinyi amesisitiza umuhimu wa Wazazi kuwahamasisha Watoto wao na Vijana ili kutekeleza Mafundisho ya Kitabu Tukufu cha Quran kwa kuisoma na kuhifadhi.

    Amewataka Walimu wanaofundisha Quran kwa njia ya Tajweed kuifikisha na kuisambaza Wilaya za Tanzania bara na Zanzibar. 

MFANYABIASHARA WA SAATENI ASHUTUMIWA KUUZA SUKARI KINYUME NA BEI ELEKEZI

    Hatua kali za Kisheria zitawachukulia kwa Wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na Bei elekezi ya Sukari iliyowekwa na Serikali .

    Tume ya Ushindani Halali wa Biashara imelifunnga Duka la  Mfanyabiashara wa bidhaa ya Sukari huko Saateni kwa  kuuza bidhaa hiyo Kinyume na Bei elekezi.

JAMII YATAKIWA KUACHA TABIA YA KUKATA MITI OVYO

    Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imewahimiza Wananchi kuendelea kuthamini juhudi za Serikali za kutunza Misitu kwa kuhakikisha Misitu inalindwa kwa maslahi yao na Taifa.

    Akizungumza katika Hafla ya Upandaji wa Mikoko katika Maeneo yaliyoathirika ndani ya Msiti wa Jozani na kuwashirikisha Wananchi katika Kijiji cha Charawe, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Shamata Shame Khamis amesema ni yema Jamii ikawa Mstari wa mbele kupinga hujuma dhidi ya Misitu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa.

SERIKALI IMESISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI ZA BIDHAA

     Serikali imesema inaendelea kusimamia sheria na kanuni kuhakikisha uzalishaji na uhamasishaji sahihi wa bidhaa unalindwa ili kumlinda Mtumiaji kutokana na mazingira.

SERA YA UCHUMI WA BULUU KURAHISISHA MAENDELEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Sera ya Uchumi wa Buluu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Dhamira ya kuimarisha uchumi wa Nchi kwa haraka. 

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Mkoa wa Mjini Magharibi alipozindua duru ya kwanza ya utoaji wa Vitalu kwa Kampuni kwenye maeneo ya Bahari kwa Zanzibar.

DKT. MWINYI AMEPOKEA SALAMA ZA POLE KUTOKA KWA KAMPUNI YA WASAFI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyiamepokea Salama za Pole kutoka kwa Kampuni ya Wasafi inayoongozwa na Mkurugenzi mkuu, Nasib Abdul (Daimond Platnum).

Dkt. Mwinyi alipokea salamu hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Kiongozi huyo na Wajumbe aliofuatana nao ameushukuru Uongozi wa Wasafi uliofika kwa lengo la kumfariji kufuatia Msiba wa Baba yake Mzazi, Mzee Ali Hassani Mwinyi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.