Habari

DIPLOMASIA YA TANZANIA IMEENDELEA KUKUA

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema katika kipindi cha Miaka Mitatu cha Uongozo wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Diplomasi ya Tanzania na Nje ya Nchi imeongezea ukilinganishwa na Miaka mingine.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kamati ya kupitia majukumu na maboresho ya Kituo cha uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kilichopo Jijini Dar es salaam ambapo amesema hali hiyo imepelekea kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Nje ya Nchini

ZAIDI YA 900 MISUNGWI WAMEPATIWA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Zaidi ya   Wakazi 900 wa Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za Matibabu ya Afya ya Kinywa na Meno zilizotolewa na wadau wa Afya katika Kituo cha Afya Usagara. 

Huduma hizo zimetolewa bure kwa wakazi wa Vijiji Vitano vya Kata ya Usagara na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Tanzania Health Environment And Development Initiative Thedi na Hope Dental Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno.

UJERMAN YAAHIDI KUIPATIA TANZANIA SHILINGI ZAIDI YA BILION 193

Jamhuri ya Shirikishso la Ujerman imesaini makubaliano na Tanzania ya kuipatia zaidi ya Shilingi Bilioni 193 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo katika Sekta ya Afya.

Makubaliano hayo yamesainiwa Jijini Dar Es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Tanzania Elijah Mwandumbya na Mwakilishi wa Serikali ya Shirikisho la Ujerman Marcus Von Essen

REA, YAZIDISHA KASI YAKE YA KUNG'ARISHA VIJIJI

       Uwanzishwaji wa Wakala wa Nishati Vijijini 'REA' umeleta Mapinduzi makubwa katika Sekta ya Nishati ya Umeme Vijijini baaada ya zaidi ya Vijiji 11,800 sawa na Asilimia 96  ya Vijiji vyote kufikiwa na Umeme na Asilimia Nne inatarajiwa kufikiwa na Umeme kabla ya Mwezi wa Sita Mwaka huu .

KAMATI ZA ULINZI ZA MIKOA KUWASAKA WIZI WA MIFUGO NA MAZAO

       Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zimehimizwa kuendelea kuwasaka na kuwakamata wanaojishughulisha na Wizi wa Mifugo na Mazao katika Jamii ili kupunguza uwepo wa Vitendo viovu Nchini pamoja na kulinda Rasilimali za Raia.

TATIZO LA TAKA LAFIKIA KIKOMO CHAKE KWA WAKAAZI WA MAGHARIB 'A'

    Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharib 'a' limejipanga kutokomeza uchafua na uzorotaji wa Taka mitaani ili kuweka haiba safi ya Wilaya hiyo.

BARAZA LA KISWAHILI YATOA TUZO YA HESHIMA KWA HAYATI MWINYI

      Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuanza kufundisha Wataalamu wa Lugha za alama ili waweze kumudu Soko la Ajira Duniani.

     Agizo hili amelitoa wakati akifungua Kongamano la Nne la idhaa ya Kiswahili Duniani linalofanyika Jijini Mbeya likijumuisha Washiriki kutoka Mataifa  mbalimbali Afrika.

WAKAAZI WA KWAHANI WALIA NA HALI YA JAA YA ENEO HILO

    Wakaazi wa Kwahani wameiomba Serikali kuwasaidia kuwawekea Dampo la kutilia Taka ili kuepusha usambaaji na ukaaji wa muda mrefu jambo linalosabisha kuenea kwa maradhi mbalimbali ya miripuko katika Maeneo yao. 

    Wakizungumza na ZBC Wakaazi wa Maeneo hayo wamesema ni muda mrefu sasa Jaa hilo lipo bila ya kuchukuliwa hatua yoyote, licha ya kuwaomba Viongozi wao wa Jimbo na Shehia bila ya Mafanikio hivyo kuwepo kwa Dampo hilo kutawasaidia Wananchi kuziweka na kuzikusanya vizuri Taka hizo.

BODI MPYA YA PBZ YAZINDULIWA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (Pbz) kuipa ushirikiano Bodi mpya ili waweze kuyapeleka mbele zaidi mafanikio ya Benki hiyo.

    Akizindua Bodi mpya ya Pbz  Dkt.Saada amesema mafanikio yaliyopatikana ni makubwa ukilinganisha na walipotoka ambapo bado kuna fursa katika Soko hivyo anaamini ushirikiano huo utawawezesha kufika lengo la Serikali.  

SMZ YAENDLELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA WANAFUNZI KUJISOMEA

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kujisomea na kufundishia ili kuzidisha ufaulu wa Daraja la Kwanza na kuhakikisha inatokomeza  Division Zero na kubaki kuwa Historia.

    Hayo yameelezwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa kukabidhi Futari kwa Wanafunzi wanaoishi Dahalia pamoja na Wananchi  wa Jimbo la Kiwani Kisiwani Pemba.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.