KAMATI ZA ULINZI ZA MIKOA KUWASAKA WIZI WA MIFUGO NA MAZAO

Kamati ulinzi na usalama

       Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zimehimizwa kuendelea kuwasaka na kuwakamata wanaojishughulisha na Wizi wa Mifugo na Mazao katika Jamii ili kupunguza uwepo wa Vitendo viovu Nchini pamoja na kulinda Rasilimali za Raia.

    Wajumbe wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake         Mhe.Machano Othman Said wametoa ushauri huo wakati walipokutana na  Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Pemba wakati wakipopkea Taarifa ya utekelezaji Wizara hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024.

    Wamesema kukithiri kwa Watu wanaofanya vitendo vya Wizi wa mifugo na mazao haviwezi kuvumilika kutokana na kurudisha nyuma juhudi za Wananchi wanyonge wanaotegemea Kilimo na Mifugo kwa ajili ya kujipatia vipato vya kuwasaidia kujikimu katika Maisha.

    Akiwasilisha Taarifa ya Wizara hiyo Afisa Mdhamini  Ndg.Thabit Othman Abdallah amesema hali ya usalama imeendelea kuimarika na Wananchi wanaendelea na shughuli  zao za kujiletea maendeleo  kwa amani na utulivu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.