Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuanza kufundisha Wataalamu wa Lugha za alama ili waweze kumudu Soko la Ajira Duniani.
Agizo hili amelitoa wakati akifungua Kongamano la Nne la idhaa ya Kiswahili Duniani linalofanyika Jijini Mbeya likijumuisha Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali Afrika.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Damasi Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita wameuomba Umoja wa Mataifa kuidhinisha na kutambua kuwa Lugha ya Kiswahili ni ya Afrika Mashariki kiasili.
Katika hatua nyingine Baraza la Kiswahili Tanzania imeikabidhi Tuzo ya Heshima kwa Familia ya Marehemu Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa Mwalimu wa Kiswahili.