TATIZO LA TAKA LAFIKIA KIKOMO CHAKE KWA WAKAAZI WA MAGHARIB 'A'

Mradi wa magari

    Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharib 'a' limejipanga kutokomeza uchafua na uzorotaji wa Taka mitaani ili kuweka haiba safi ya Wilaya hiyo.

    Akizindua Mradi wa Gari za kubebea taka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Muhammed amesema Baraza la Manispaa linawajibu wa kuzitumia Gari hizo kwa makusudio ili kuondosha tatizo la urundikaji wa Taka Mitaani ili kuweka mazingira salama na kuwataka Viongozi wa Baraza hilo kushirikiana na Wananchi ili kuhakikisha malengo ya kung’arisha Mji yanafikiwa .

    Mkurugenza Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharib 'a'  Ndg.Mbaraka Said Hassuni amesema Baraza litahakikisha linatumia Gari hizo kama ilivyo kusudiwa ili kuondokana na Tatizo la Taka huku akisisitiza Wananchi kulipia Taka ili kuendeleza kudumisha uhai wa Gari hizo pamoja na kuchangia katika mendeleo mbalimbali ya Wilaya.

   Meneja wa Tawi la Amana Bank Zanzibar Ndg.Suleiman Suleiman amesema Bank hiyo imekuwa na ushirikiano kubwa na Serikali ya Zanzibar katika kuhakikisha maendeleo yanafikiwa kwa haraka amesema Bank hiyo imekuwa ikitoa Mikopo bila ya riba kutokana na kufata misingi ya Kiisilamu.

   Mradi huo wa Gari za Taka umejumuisha Gari Tatu na Kijiko kimoja kwa Mkopo wa Milioni Mianane na Thalathini kutoka Amana Bank.

                                                             

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.