Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kujisomea na kufundishia ili kuzidisha ufaulu wa Daraja la Kwanza na kuhakikisha inatokomeza Division Zero na kubaki kuwa Historia.
Hayo yameelezwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa kukabidhi Futari kwa Wanafunzi wanaoishi Dahalia pamoja na Wananchi wa Jimbo la Kiwani Kisiwani Pemba.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa Elimu na hali halisi ya maisha ya Dahalia wameona ipo haja ya Kuftari pamoja na Wanafunzi wanaoishi Dahalia kwa kuwapatia futari ambayo itawasaidia ili Wanafunzi kubakiwa na kazi moja tu ya kusoma kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha Makamuo wa Pili wa Rais amewataka Wanafunzi kuongeza bidii katika Masomo yao ili kupata Viongozi bora na wenye kuelimika ambao watakuja kulitetea taifa kwa kuendeleza miradi ya kimaendeleo kuitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuhakikisha wanapeleka Walimu wa kutosha katika Skuli ili kupata Matokeo mazuri kwa Wanafunzi hasa wa Kidato cha Nne na cha Sita.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohamed Mussa amemshukuru Makamo wa Pili wa Rais kwa kukuendelea kuwasaidia Wanafunzi wanaoishi katika Dahalia kwa kuwapatia Ftari jambo ambalo linatoa ahuweni ya maisha kwa Wanafunzi hao na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu Siku hadi Siku.
Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiwani Mauwani wameishukuru Serikali ya Awamu ya Nane (8) kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kujifunzia pamoja na kuwapatia mahitaji ya lazima ikiwemo Ftari kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Wakati huo huo Makamo ya wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekabidhi Ftari kwa Wananchi wote wa Shehia Nne(4) zilizomo katika Jimbo la Kiwani ili iliyotolewa na Mfanya Biashara maarufu Zanzibar Ndugu Said Nassir Nassor ( Bopar) kwa lengo la kuwasaidia Wananchi wa Jimbo hilo.
Skuli zilizokabidhiwa Ftari na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni pamoja na Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua, Skuli ya Sekondari ya Ufundi Kengeja na Skuli ya Sekondari Mauwani Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.