Habari

MH. HEMED AMEWAASA WANAFUNZI KUZIDISHA JUHUDI KATIKA MASOMO YAO.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewaasa Wanafunzi wa Kidato cha Sita  kuzidisha juhudi katika Masomo yao ili kupata Viongozi bora wa baadae. 

Ameyasema hayo wakati akikabidhi Futari kwa Wanafunzi wanaoishi Dahalia mbali mbali Kisiwani Pemba kwa lengo la kuwarahisishia upatikanaji wa Ftari katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

NCHI ZA AFRIKA KUCHUKUWA HATUA ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI.

Nchi za Afrika zimetakiwa kuchukuwa hatua madhubuti za utunzaji wa Mazingira kwa kupanda Miti ili kuepuka Madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya Tabia ya Nchi yakiwemo mafuriko yanayoharibu kingo za mito na kusababisha Mmomonyoko wa Ardhi

WIZARA YA AFYA ITASHIRIKIANA NA MASHIRIKA KUONDOA MALARIA

Wizara ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Mshirika ya Kimataifa na Wadau wengine kuhakikisha kuwa Maradhi ya Malaria yanaondoka hapa Nchini.

MISAADA YA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA NA WAZEE NI ALAMA YA IMANI KATIKA JAMII.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh Ana Atanas Paul amesema kuwepo kwa Misaada mbalimbali ya kuwasaidia Watoto Yatima na Wazee ni Alama ya Imani na Ushirikiano kwa Watu hao. 

Akikabithi Msaada wa Chakula kwa Niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika Vituo vya kulelea Watoto Yatima na Wazee wasiojiweza amesema Serikali inatambua Thamani ya Makundi hayo katika kuwawezesha kwa kuwapatia Msaada stahiki katika Vituo vyao.

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA KUPUNGUZA VIHATARISHI VYA MAAFA NCHINI

Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeihimiza  Kamisheni ya kuakbiliana na  Maafa Nchini kuendelea kuweka Mikakati Madhubuti katika kujiandaa na kukabiliana na maafa pindi yanapotokea ili kupunguza vihatarishi vya maafa Nchini.

Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe Machano Othman Said wametoa ushauri huo wakati wakipokea Taarifa ya  Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wete Pemba.

SERIKALI YAZIAGIZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI KUDHIBITI UPOTEVU WA MAJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeziagiaza Mamlaka za Maji Nchini kuhakikisha zinadhibiti Upotevu wa Maji na kuhakikisha wanaimarisha upatikanaji wa Maji kwa Wananchi sawa na uwekezaji mkubwa na unaofanywa na Rais Samia.

Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri wakati akizindua Ripoti ya Tathamini  ya Utendaji Kazi wa Mamlaka za Majisafi na usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.

MHE.DOTO BITEKO ASHIRIKI MISA YA KUMUOMBEA HAYATI MAGUFULI

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuendelea Kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa matendo mema kwa Watanzania na amesema  Serikali  itaendeleza yale aliyoyaacha.

    Amesema hayo katika Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mt. Yohana Maria Muzeyi Wilaya  ya Chato, Mkoa wa Geita.

WAZIRI HAMZA AWATAKA WANANCHI KUACHA UJEZNZI HOLELA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mh.Hamza Hassan Juma amezitaka Mamlaka za kudhibiti Maafa kuchukuwa hatuwa za haraka kwa Wananchi wanaojenga ujenzi holela.

    Akizungumza katika Ziara ya kukaguwa Maeneo yalioathirika na Mvua Wilaya ya Magharibi "a" Mhe.Hamza amesema kufanya hivo kutanusuru Maafa ambayo husababishwa na Mvua na kupelekea kukosa Maakazi.

DKT.KHALID AKAGAUA BARABARA YA FUONI TUNGUU

    Wananchi wameshauriwa kuachana na utaratibu wa Kujenga katika Maeneo ya hakiba ya Barabara kwani kufanya hivyo ni  kinyume na sheria  na inaondoa haiba za Barabara na Mji.

     Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati wa  Ziara ya kukaguwa Barabara ya Fuoni Daraja la Shein hadi Barabara ya Tunguu yenye urefu wa Kilomita 5.8.

     Dkt. amesema  Barabara baadhi ya Wananchi wanajenga kwenye sehemu hizo jambo ambalo ni  kinyume na sharia 

KANDA YA ZIWA WAFIKIWA NA HUDUMA YA MAGONJWA YA MOYO

     Zaidi ya Watu Milioni 22 wa Kanda ya Ziwa wamerahisishiwa huduma ya Magonjwa ya Moyo na matibabu ya kibingwa kufuatia Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.

     Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Hospitalini hapo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, huku akiweka bayana lengo la kuanzishwa kwa Hospitali hiyo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.