Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeziagiaza Mamlaka za Maji Nchini kuhakikisha zinadhibiti Upotevu wa Maji na kuhakikisha wanaimarisha upatikanaji wa Maji kwa Wananchi sawa na uwekezaji mkubwa na unaofanywa na Rais Samia.
Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Maji Mhandisi Mwajuma Waziri wakati akizindua Ripoti ya Tathamini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka za Majisafi na usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Kwa upande Wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James andilile amesema pamoja na kuimarika kwa Utendaji kazi wa Mamlaka za Maji katika kutoa huduma,Uchambuzi umebainisha changamoto zinazozikabili Mamlaka hizo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Omar Ali Yussuf,amesema kuwa EWURA imekuwa ikifanya kazi kubwa ambayo inaleta heshima kwa Taifa la Tanzania.