Habari

WAMASAI ZANZIBAR WATOA UBANI WAO KWA DKT.MWINYI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamasai wanaoishi Zanzibar Ndg.Ereto Thomas Makau Lepachu na Ujumbe wake kufuatia Kifo cha Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

DKT.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM

    Makamu Mwenyekiti wa CCM  Zanzibar, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi Amepokea salamu za pole kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wa Zanzibar wakiongozwa na              Ndg. Mohamed Aboud Mohamed waliofika Ikulu Mnazi Mmoja.

    Wajumbe hao wa Kamati Kuu ya CCM Zanzibar wamesema Msiba huu ni wa wote kwani Marehemu alikuwa amewafundisha wengi mazuri kwa Taifa.   

USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI KIGEZO CHA UTAWALA BORA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfumo wa Sema na Rais SNR  ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Wananchi na kigezo muhimu cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji wa Wananchi.

     Dk. Mwinyi alieleza hayo katika maadhimisho ya Miaka Mitatu ya Mfumo wa Sema Na Rais Mwinyi katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.Alisema kupitia SNR, Serikali imefanikiwa kuongeza ukaribu na Wananchi kwa kuzisikiliza matatizo yanayowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.   

VIWANDA VYA KUSINDIKA SAMAKI MARA VYAFUNGWA

    Viwanda vya kusindika Samaki vyafungwa kutokana na kukosa malighafi licha ya Mkoa wa Mara kuwa na asilimia  36 ya Ziwa Victoria jambo ambalo limepekea Mkoa huu kukosa Viwanda vikubwa .

    Awali akisoma Taarifa ya hali ya Viwanda katika Mkoa wa Mara katika Baraza la Biashara Mkoa  Afisa Biashara Mkoa Gambaless Timotheo amesema kukosekana kwa Samaki kumepleka kufungwa kwa Viwanda Vinne ambavyo vilikuwa vikisindika Samaki hao.

RC AYOUB ATAKA SHEREHE ZA MWAKA KOGWA KUTANGAZWA KIMATAIFA

    Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja  Ayoub Mohammed Mahamoud ameitaka Kamati ya Sherehe za Kijadi za Mwaka Kogwa  kuzitangaza Sherehe hizo Kimataifa  ili zilete tija  kwao na kwa Taifa.

    Akizungumza na Wazee wa Kamati ya Mwaka Kogwa Makunduchi Mkuu huyo wa Mkoa amesema  Tamasha hilo la muda mrefu lakini halijatangazwa kama yalivyo Matamasha mengine Duniani.

TAMWA YAFANYA TATHMINI YA TUNZO ZA WAANDISHI WA HABARI

    Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kimewashauri Wahariri wa Vyombo vya Habari kuzipitia kazi zinazowasilishwa katika Tunzo za Takwimu za Wanawake na Uongozi ili ziweze kuwa na ubora.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Majumuisho ya Hafla ya utoaji tunzo zilizotolewa hivi karibuni,  Mkurugenzi  wa TAMWA, Zanzibar, Dkt.Mzuri Issa, amesema baadhi Waandishi wa Magazeti na Redio, waliowasilisha kazi zao, hazikuwa na kiwango cha kuridhisha kutokana na kutopitiwa na Wahariri. 

WAZIRI JAFO ATOA SIKU 14 ZA KUFANYA TATHMINI YA KIMAZINGIRA DODOMA

      Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo, ametoa Siku 14 kwa Ofisi ya Madini Mkoa wa Dodoma, Jiji la Dodoma pamoja na Baraza la Taifa la uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini ya uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchimbaji kokoto na kifusi katikati ya Jiji kinyume na Sheria ya mazingira.

    Waziri Jafo ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma mara baada ya kufanya Ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini ya Ujenzi aina ya kokoto na Kifusi katika eneo la Iyumbu na Njedengwa.

HALMASHAURI WATAKIWA KUTUMIA MAPATO YAO KUAJIRI WATUMISHI

    Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ili kupunguza tatizo la uhaba wa Watumishi wa Sekta ya Afya linalozikabili baadhi ya Wilaya amezielekeza Halmashauri za Wilaya na Hospitali Nchini kutumia mapato yao ya ndani kuajiri Watumishi wa Kada hiyo kwa Mikataba.

    Waziri Ummy ameyasema hayo Jijini Mwanza wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi ilipotembelea Mradi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

DKT.SAMIA AWATAKA WANAWAKE KUTOKUBALI KUKATISHWA MALENGO YAO

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amekitaka Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha TAWIFA, kuzingata miongozo ya Chama hicho waliojiwekea na kuzingatia Demokrasia, pamoja na kulipa kipaumbele suala la kumuwezesha Mwanamke kiuchumi ili kumkomboa kimaisha. 

WAFANYA BIASHARA WAASWA KUTOFICHA SUKARI

Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Ushindani halali wa Biashara Mohammed Sijamini Muhammed amesema kufuatia Ukaguzi walioufanya  leo  na Tume hiyo imebaini kuwa  wapo baadhi ya Wafanya Biashara wamekuwa wakificha Bidhaa ya Sukari na wengine kuuza  kinyume na Bei elekezi iliyotangazwa na Serikali.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.