USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI KIGEZO CHA UTAWALA BORA

Miaka mitatu ya sema na Rais

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfumo wa Sema na Rais SNR  ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Wananchi na kigezo muhimu cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji wa Wananchi.

     Dk. Mwinyi alieleza hayo katika maadhimisho ya Miaka Mitatu ya Mfumo wa Sema Na Rais Mwinyi katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.Alisema kupitia SNR, Serikali imefanikiwa kuongeza ukaribu na Wananchi kwa kuzisikiliza matatizo yanayowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.   

     Amebainisha kuwa kupitia Mfumo huo Serikali inapata fursa ya kupokea maoni na ushauri wa Wananchi kuhusiana na maendeleo na ustawi wa Jamii na kuyazingatia.   

     Amesema katika Kipindi cha Miaka Mitatu, Zaidi ya Malalamiko 13,00- yameweza kupokelewa na kati ya hayo 11,000 sawa na Asilimia 82.6 yameweza kupatiwa ufumbuzi huku malalamiko 2,351 sawa na Asilimia 17.4 yanaendelea kufanyiwa kazi.        

     Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe, Ali Suleiman Mrembo, amesema Rais Mwinyi ni Kiongozi mwenye bahati kwa Wananchi kwa ubunifu, maarifa, uthubutu na uvumilivu wa Kumuabudu Mungu kuwa chachu na dira ya mafanikio  ya Zanzibari. 

     Mapema Naibu Mkurugenzi wa SNR Ndg. Haji Khamis akitoa  Taarifa ya Mfumo huo amesema Mwaka 2021 wamepokea malalamiko 6,773 na yametatuliwa 4,571 

      Kwa Mwaka 2023/2024 Jumla ya Malalamiko 13,517 yameshapokelewa na malalamiko 11,116 yamepatiwa utatuzi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.