Habari

SERIKALI KUKEMEA VIKUNDI VYA RUSHWA NA UBADHIRIFU

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi Binafsi katika kujenga Uchumi imara pamoja na  kuwachukulia hatua  wanaohusika na Ubadhirifu, Rushwa na Ufisadi.

Akifungua Mkutano Mkuu wa  Mwaka wa kupambana na Rushuwa na Ufisadi  kwa Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu wa Taasisi Binafsi na za Umma juu ya masuali ya ubadhirifu na Rushwa ambapo amesema uchumi imara hujengwa kwa mtazamo na Vitendo vyema visivyo kuwa na Rushwa.

AAKIA KUSHINDA TUZO YA UWANJA BORA

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume  imeshinda Tunzo ya Uwanja bora wa Ndege Barani Afrika unaotoa huduma bora kwa Abiria.

Tunzo hizo zinazotolewa kila Mwaka za Viwanja bora zinazotambua ubora wa Uwanja kupitia maoni ya Abiria Duniani kote kwa tafiti maalum zinazofanyika kwa Abiria katika maeneo ya kuondokea na kuwasili Abiria.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa uhusiano Mulhat Yussuf amesema Mamlaka inatarajia kupokea Tunzo hiyo Septemba Mwaka huu katika Mkutano na maonyesho kwa huduma ya Wateja Duniani.

 

MRADI WA KUFUNGA KIFAA MAALUMU KATIKA MELI ZA UVUVI WASAINIWA

     Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu wamesaini hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka hiyo na Mradi wa Usaid Heshimu Bahari  Chemonic International INC ili kuimarisha usimamizi wa Rasilmali za Bahari kwa kufunga kifaa maalumu kitakachoonyesha uhalisia wa sehemu utakayovua.

    Wakisaini  Hati ya Ushirikiano  huo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ndg. Emanuel Andrew Sweke amesema Kifaa hicho  kitasaidia  Sekta ya Uvuvi kupunguza kuvua Uvuvi haramu na kuzuwia mianya ya upotevu wa rasilmali za bahari zisipotee.

VIFO VYA WALIOKULA KASA WIZARA YA AFYA YATOA RIPOTI

    Wizara ya Afya Zanzibar imetoa Ripoti ya Utafiti uliofanywa kufuatia Watoto Tisa 9 kufariki Dunia na wengine wakiendelea kupatiwa Matibabu baada ya kusadikiwa Kula Nyama ya Kasa ambayo imesababisha madhara makubwa

    Akitoa Ufafanuzi wa Rripoti hio Naibu Waziri Wizara ya Afya Hassan Khamis Hafidh amesema Tukio hilo limeripotiwa Marchi 6 katika Kijiji cha Kisiwa Panza Mkoa wa Kusini Pemba  na Watu wengine Takriban 160 wameathirika na Nyama hiyo na kupatiwa Matibabu, 

CHINA YAISAIDIA ZANZIBAR KATIKA KAMPENI YAKE YA KUWEKA MJI SAFI

     Jamhuri ya Watu wa China imesema Watalii wengi wa China wamehamasika kutembelea Zanzibar kutokana na mandhari iliyopo na Utamaduni wa Asili wa Watu wake.

    Akikabidhi Vifaa vya Usafi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed kwa ajili ya Manispaa ya Mjini, Kaimu Balozi Mdogo wa China aliepo Zanzibar Bw. Zhang Ming, amesema ni jambo la faraja kuona Mji wa Zanzibar unaendelea kuwa safi na kuwa kivutio kwa Wageni wengi zaidi

MPANGO WA KUMALIZA UKIMWI ZANZIBAR KUANDALIWA

     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema  ni fursa muhimu  kwa Nchi kuwepo mpango endelevu wa kitaifa katika kupambana na maambukizo na maradhi ya Ukimwi.

    Mhe. Othman ameyasema hayo Ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar alipozungunza na Ujumbe wa Washirika wa wa Maendeleo uliongozwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS), Mfuko wa Rais wa Marekani   pamoja na Taasisi ya Marekani ya kudhibiti Maradhi mbali mbali.

FURSA ZA KUJIFUNZA KICHINA ZAWAFIKIA WANAFUNZI SUZA

    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzbar Mhe. Lela Mohamed Mussa  amewasisitiza Wanfunzi kusoma Lugha za Kigeni ili kupata fursa mbalimbali zanazopatika kotokana na ujuzi wa lugha hizo 

    Amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Darasa la Kichina Chuo Kikuu Cha Zanzibar SUZA na kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo itawasaidia wao  kupata fursa mbalimbali za kusoma Nje ya Nchi na Ajira kupitia kujifunza lugha hiyo 

POLE HAZIJAMALIZA KUMIMINIKA KWA DKT.MWINYI

    Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea Salamu za Pole kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara  Abdulrahman Omar Kinana.

    Kinana ametoa Pole hiyo Ikulu Zanzibar, amemueleza Rais Dkt. Mwinyi kuwa Mmsiba  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Awamu ya Pili umewagusa Watu Ndani na Nje ya Tanzania.

RAIS MWINYI AMETOA SHUKRANI KWA WANANCHI WA TAASISI ZOTE ZILIZOMUOMBEA DUA MZEE ALI HASSAN MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa Shukrani kwa wale wote wanaomuombea Dua Marehemu Rais Mstaafu wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi tokea alipofariki Tarehe, 29 Februari 2024 hadi leo.

SMZ NA SMT KUTAMBUA MCHANGO WA WANAWAKE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili za Tanzania zinatambua umuhimu na mchango mkubwa wa Wanawake katika hatua mbalimbali za maendeleo ikiwemo kumlinda na kumwezesha Kiuchumi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.