Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema ni fursa muhimu kwa Nchi kuwepo mpango endelevu wa kitaifa katika kupambana na maambukizo na maradhi ya Ukimwi.
Mhe. Othman ameyasema hayo Ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar alipozungunza na Ujumbe wa Washirika wa wa Maendeleo uliongozwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS), Mfuko wa Rais wa Marekani pamoja na Taasisi ya Marekani ya kudhibiti Maradhi mbali mbali.
Ujumbe huo ulikuwa na dhamira ya kumueleza Mhe. Makamu juu azma ya Mashirika hayo na umuhimu wa Nchi kushirikiana na Mashirika hayo kuisaidia Zanzibar kuwa na mpango endelevu wa kupambana na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
Mhe. Othman amesema kwamba kuwepo kwa Mpango huo kutaisadia sana Zanzibar kuweza kupiga hatua na kuwepo mafanikio mazuri ya vita dhidi ya Janga la Maradhi ya Ukimwi na kusaidia kufikia lengo la Kimataifa la kumaliza matatizo ya Ukimwi ifikapo Mwaka 2030.
Mshauri wa Shirika la Umoja wa Matifa la kupambana na Ungonjwa wa Ukimwi Duniani ( UNAIDS) Dk. Gorge Loy, amesema Washirika wa maendeleo wa kupambana na Maradhi hayo wataendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuandaa na kuwepo na mpango endelevu utakaotumika kumaliza tatizo la Ukimwi Zanzibar.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Saada Mkuya amesema kwamba Kamati hiyo itasaidia katika kuyakabili mazingira tofauti ya kuweza kupambana na tatizo la Ukimwi Nchini .
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Kkhatib amesema kwamba mpango endelevu wa kupambana na Ukimwi Zanzibar ni shirikishi kwa jitihada za Wadau tofauti wa maendeleo kama ni jitihada ya pamoja ya kupamba ikiwemo Shirika