Habari

SERIKALI ITAENDELEA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUTUMIA NISHATI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuwawezesha Watanzania kutumia Nishati safi ya kupikia ili ifikapo Mwaka 2030 zaidi ya asilimia 88  wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia.

Ameyasema hayo  alipozungumza kwa njia ya Simu na Wanawake waliojitokeza katika Kongamano la kumpongeza kwa kuwa kinara wa Nishati safi ya Kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto yaliyofanyika katika Ukimbi wa Diamond Jubelee Dar Es Salaam, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi.

WAISLAMU WAHIMIZWA KUTOA SADAKA KWA YATIMA.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said amewataka Waislamu  kuendelea kujitokeza kuwasaidia  Watoto Yatima ili kupata mahitaji ya kila siku ikiwemo Futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 

Akizungumza katika Hafla ya kuwachangia  Watoto Yatima walioko Majumbani  iliofanyika huko katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja Ndege  amesema kufanya hivyo kutawawezesha Watoto hao kuwa na uhakika wa Chakula na huduma nyengine.

SMZ KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA NORWAY KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI YA UMEME ZNZ

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Norwey inajipanga kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa Nishati ya Umeme utakaokuwa wa uhakika na endelevu Mjini na Vijijini. 

ZASCO YASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA NMB

Kampuni ya Mwani Zanzibar (Zasco) imeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya NMB wenye lengo la kuwawezesha Wakulima zaidi ya 23,000 wa Zao la Mwani Visiwani Zanzibar ili waweze kuzalisha kwa ubora na tija.

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano hayo Jijini Dar Es Salaam Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omari Said Shaaban amesema Makubaliano hayo yanakwenda kufanya Mapinduzi na Kupelekea kuinua uchumi wa Mwanamke pamoja na Kuingizia Nchi Fedha za Kigeni na kutoa ajira kwa Wazanzibar.

DKT.BITEKO AWAONYA WATUMISHI KUACHA USUMBUFU KWA WAWEKEZAJI

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko,amewaonya Watendaji na Watumishi wa Umma wanaoendekeza Vitendo vya Urasimu na kuleta usumbufu kwa Wawekezaji wanaotaka kuwekezaji hapa Nchini.

    Dkt.Biteko ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati akizindua Rafiki Dodoma Hotel ambapo amesema kuwa Serikali inafanya kazi kubwa kuvuta Wawekezaji lakini kuna baadhi ya Watendaji wanakwamisha.

WANAHABARI WATAKIWA KUZIPA KIPAUMBELE HABARI ZA UDHALILISHAJI NA UKATILI WA WANAWAKE

     Waandishi wa Habari Nchini wametakiwa kuandika Habari zinazohusu vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto, ambavyo vimekuwa na athari katika Jamii.

    Akikabidhi Tunzo za umahiri wa Uandishi wa Habari za Takwimu za Vitendo hivyo, katika Skuli ya Shaa Mombasa, Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Ndg.Salum Kassim Ali, amesema Uandishi huo uzingatie vigezo ili kuweza kuleta mabadiliko dhidi ya vitendo hivyo.

SERIKALI YATAJA BEI ELEKEZI KWA SUKARI UNGUJA NA PEMBA

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imeweka Bei elekezi kwa bidhaa ya Sukari ili kuwapa Wananchi unafuu wa maisha  hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan .

     Akizungumza na vyombo vya Habari Waziri wa Biashara Maendeleo ya Viwanda Mhe Omar Said Shaaban amesema hatua hiyo itawasaidia Wananchi kwa kuwapunguzia kodi ya ushuru ili na wawe waweke bei ya bidhaa ya Sukari iweze kuwa chini ili kila mmoja aweze kuimudu kwa bei ya unafuu.

ZBC YADHAMINI MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QUR-AN AFRIKA

    Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amesema Mashindano ya Kuhifadhisha  Qur-an  yana mchango mkubwa katika kuwajenga Vijana Kimaadili, fikra na nidhamu pamoja na kumjua Mwenyezi Mungu.

     Ameyasema hayo katika Uzinduzi wa Mashindano ya Kimataifa  ya Qur-an Tukufu uliofanyika katika Ukumbi wa Madinatul Bahar Mbweni Jijini Zanzibar.

DKT.MWINYI ATOA PONGEZI NYINGI KWA VIKOSI VYA KMKM NA KVZ

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Maafisa, Askari na Wapiganaji wa Vikosi vya SMZ kuendelea kudumisha nidhamu, uzalendo , uwajibikaji na uadilifu.

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Maafisa , Askari na Wapiganaji wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Kibweni na Kikosi cha KVZ Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mwendelezo wa Ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ. 

DKT.MWINYI AZUNGUMZA NA WAPIGANAJI WA VIKOSI VYA SMZ

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha Vikosi vya SMZ.

    Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Wapiganaji wa Vikosi vya SMZ, akiwa katika Ziara ya kuvitembelea Vikosi hivyo huko Kitogani,Hanyegwa Mchana na Saateni.

    Akizungumzia Kikosi cha Zima Moto na Uokozi Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali tayari imeshazungumza na Kampuni ambayo yataweza kuwapatia vifaa vya kazi kwa ajili ya Kikosi hicho .

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.