Kampuni ya Mwani Zanzibar (Zasco) imeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya NMB wenye lengo la kuwawezesha Wakulima zaidi ya 23,000 wa Zao la Mwani Visiwani Zanzibar ili waweze kuzalisha kwa ubora na tija.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano hayo Jijini Dar Es Salaam Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omari Said Shaaban amesema Makubaliano hayo yanakwenda kufanya Mapinduzi na Kupelekea kuinua uchumi wa Mwanamke pamoja na Kuingizia Nchi Fedha za Kigeni na kutoa ajira kwa Wazanzibar.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Benki ya NMB Filbert Mponzi amesema wakulima wa Mwani Watapatiwa Elimu ya Fedha na kilimo cha Mwani ili uzalishaji wao uwe na manufaa zaidi kwa uchumi wao Binafsi na Nchi kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa ZASCO Dkt Masoud Rashid Mohammed licha ya kushukuru, amesema makubaliano hayo yanaendea kuendeleza zao la Mwani Visiwani Zanzibar.