Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha Vikosi vya SMZ.
Dk. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Wapiganaji wa Vikosi vya SMZ, akiwa katika Ziara ya kuvitembelea Vikosi hivyo huko Kitogani,Hanyegwa Mchana na Saateni.
Akizungumzia Kikosi cha Zima Moto na Uokozi Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali tayari imeshazungumza na Kampuni ambayo yataweza kuwapatia vifaa vya kazi kwa ajili ya Kikosi hicho .
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed amemuhakikishia Rais Mwinyi kuwa Vikosi hivyo vinaendelea na Majukumu yake kama ilivyoainishwa na sheria ya Nchi pamoja na kulinda amani ya Nchi.
stories
standard