Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Maafisa, Askari na Wapiganaji wa Vikosi vya SMZ kuendelea kudumisha nidhamu, uzalendo , uwajibikaji na uadilifu.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na Maafisa , Askari na Wapiganaji wa Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Kibweni na Kikosi cha KVZ Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mwendelezo wa Ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ.
Dk.Mwinyi amewapongeza Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Kikosi cha KVZ kwa kutekeleza kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo inayofanywa na Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya Vikosi hivyo.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed amesema Vikosi hivyo vitaendelea kulinda amani,heshima,utu wa Nchi pamoja na kulinda msingi wa uhuru ambayo ni Mapinduzi ya Januari 1964.
Komodoo Azzan Hassan Msingiri amesema KMKM itaendelea kuwa wazalendo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Nae Kamanda Mkuu wa KVZ Luteni Kanali Said Ali Juma Shamhuna amemuelezea Dkt. Hussein majukumu ya Kikosi hicho ambayo yanatekeleza kwa ufanisi na uweledi