Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said amewataka Waislamu kuendelea kujitokeza kuwasaidia Watoto Yatima ili kupata mahitaji ya kila siku ikiwemo Futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Akizungumza katika Hafla ya kuwachangia Watoto Yatima walioko Majumbani iliofanyika huko katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja Ndege amesema kufanya hivyo kutawawezesha Watoto hao kuwa na uhakika wa Chakula na huduma nyengine.
Amesema msaada unaaotolewa kwa Yatima unasaidia kuwapa Faraja na kukumuwesha mtowaji kufuata mwenendo wa Dini yako
Kiongozi wa Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Orphans Trust Tanzania Mhandisi Salha Muhammed Kassim amesema lengo ka shughuli hiyo ni kuwachangia Watoto hao ili waondokane na upweke
Shekh Hassan Al Basary kutoka Kenya ameitaka Jamii kuwatambua Yatima kwa kuwafanyia wema na ukarimu kwa kutoa walivyo navyo ili waweze kufarijika na kuweza kuwakidhia haja zao
Akitoa Salamu za Wadhamini Muakilishi kutoka PBZ Salim Hassan Iddi amesema sadaka kwa Watoto Yatima ,wasiojiweza na wengine waliotajwa katika Kitabu kitukufu ni muhimu kwa kila mwenye uwezo kwani huzitakasa Mali zao na kuwa Radhi mola wao.