WAISLAMU WAHIMIZWA KUTOA SADAKA KWA YATIMA.

MHANDISI ZENA AHMED SAID

Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said amewataka Waislamu  kuendelea kujitokeza kuwasaidia  Watoto Yatima ili kupata mahitaji ya kila siku ikiwemo Futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 

Akizungumza katika Hafla ya kuwachangia  Watoto Yatima walioko Majumbani  iliofanyika huko katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja Ndege  amesema kufanya hivyo kutawawezesha Watoto hao kuwa na uhakika wa Chakula na huduma nyengine.

Amesema msaada unaaotolewa kwa Yatima unasaidia kuwapa Faraja na kukumuwesha mtowaji kufuata mwenendo wa Dini yako

Kiongozi wa Mkuu wa Taasisi ya Taqwa Orphans Trust Tanzania Mhandisi Salha  Muhammed Kassim amesema lengo ka shughuli hiyo ni kuwachangia Watoto hao ili waondokane na upweke 

Shekh Hassan Al Basary kutoka Kenya ameitaka Jamii kuwatambua Yatima kwa kuwafanyia wema na ukarimu  kwa kutoa walivyo navyo  ili waweze kufarijika na  kuweza kuwakidhia haja zao 

Akitoa Salamu za Wadhamini Muakilishi kutoka PBZ Salim Hassan Iddi amesema sadaka kwa Watoto Yatima ,wasiojiweza na wengine waliotajwa katika Kitabu kitukufu ni muhimu kwa kila mwenye uwezo kwani huzitakasa Mali zao na kuwa Radhi mola wao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.