Habari

UTAPENDA JINSI WANAWAKE WA TRA ZANZIBAR WALIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

    Mhe.Wanu Hafidh Ameir amewahimiza Wanawake kuendelea kutoa malezi kwa Jamii ili kuwa na maadili mazuri.

     Mhe.Wanu amesema hayo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Wanawake wa TRA kukabidhi msaada kwa Kituo cha Assalam Orphans Center.

    Amesema kuwa kulea Yatima kunahitaji moyo na ni jambo kubwa kwa Mwenyezi Mungu. amesema kuwa Wanawake wa TRA wameweza kufanya jambo kubwa kwa kutoa na kuwatizama Watoto Yatima.

DK.MWINYI AWAAPISHA MAKATIBU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU ZANZIBAR

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ,  amewaapisha  Makatibu, Manaibu Makatibu Wakuu na Mhasibu Mkuu wa Serikali aliowataeua hivi karibuni.

      Hafla hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama na Vikosi vya Ulinzi na Usalama,

  Walioapishwa ni makatibu wakuu,  manaibu katibu wakuu na mhasibu mkuu wa serikali. Nao ni -;

Makatibu Wakuu

KUWEPO KWA HAKI SAWA YA KIJINSIA KUMESAIDIA KUKUZA UCHUMI WA NCHI

    Kuwepo kwa haki sawa ya Kijinsia katika utendaji kazi kumechangia maendeleo imara ya kiuchumi.

    Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma amesema maadhimisho hayo ni ishara ya Maendeleo ya kiutendaji katika Serikali hali ambayo imechangia kukua kwa Sekta mbalimbali Serikalini kwa kuwepo kwa haki ya usawa wa jinsia katika nafasi mbalimbali za Uongozi.

POLISI WANANDOA WALIOFARIKI KWA AJALI WAFANYIWA IBADA

     Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wamefanya ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea Askari Polisi Wanandoa Waliofariki Dunia kwa ajali ya Gari Siku Mbili baada ya kufunga Ndoa.

CHINA YAENDELEA KUSAIDIA HUDUMA ZA MATIBABU ZANZIBAR

     Jumla ya Watoto 400 wa Skuli ya Maandalizi ya Kidutani wamepatiwa huduma ya upimaji wa afya ili kuhakikisha wanakuwa na Afya njema

JOKATE; DKT. SAMIA NDIO KIELELEZO NA KINARA KWENYE UONGOZI

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jokate Mwegelo amewataka Wanawake Nchini kujitokeza Kugombea Nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024na ule Mkuu wa Mwaka 2025.

     Mhe.Jokate ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wanawake wa Mkoa wa Dar-es-salaam ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo amewataka Wananwake kujitokeza kushiriki katika maadhimisho hayo.

HUZUNI :WATOTO NANE WAFARIKI BAADA YA KULA SAMAKI AINA YA KASA

    Watoto  Wanane  Wakaazi wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani Wamefariki Dunia baada ya Kudhaniwa Wamekula Samaki aina ya  Kasa akiwa na sumu.

      Wakizungumza kwa masikitiko  makubwa   baadhi ya Wahawanga  wa Tukio hilo akiwemo Ndg.Miza Kombo Bakari  ambaye alipoteza Watoto wake Wawili  Mmoja wa Miaka Miwili na Nusu na mwengine wa Miezi Mitano  amesema hakufahamu chanzo cha tukio hilo.

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOA WA MWANZA WAFANYA JAMBO

    Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Mwanza wamewataka Wanawake wa Mkoa huo kuhakikisha wanatenga muda wa Malezi kwa Watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Majumbani

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZSSF YAIADHIMISHA KWA VITENDO

     Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani umetoa Vifaa kwa Mama na Watoto waliozaliwa.

    Akizungumza katika hafla hiyo kwa Niaba ya ZSFF Ndg.Zainab Rajab Baraka amesema lengo la kufanya hivyo ni kuthamini mchango wa Wanawake katika Jamii hasa katika vikwazo vinavyowakumba na kuweza kukabiliana navyo

MABADILIKO YA KASI YAHITAJIKA PBZ

    Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, imeitaka Benki ya Watu wa Zanzibar Pbz kubadilika ili kwenda kwa kasi zaidi na kufikia malengo ya Serikali.

    Akijitambulisha kwa Uongozi wa Benki ya Pbz Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juma Makungu Juma amesema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana na Benki hiyo bado ipo nyuma katika utoaji wa huduma ukilinganisha na Benki nyengine zilizoanzishwa hivi karibuni ambazo zinaonekana kuwa juu.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.