Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Mwanza wamewataka Wanawake wa Mkoa huo kuhakikisha wanatenga muda wa Malezi kwa Watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Majumbani
Wakizungumza katika Kituo cha Malezi cha Foundation Karibu Tanzania FKT kilichopo Kiloleli Wilaya ya Ilemela, Mtandao huo wa Polisi Wanawake TPF-NET wamesema lengo la kuwapa mahitaji maalum Watoto hao ni wale waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji Majumbani kwao mbali na kutoa mahitaji ya Chakula kwa Watoto hao pia wamewakumbusha Wazazi hasa kina mama kuwa makini na malezi ya Watoto wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho cha malezi kwa Watoto cha Foundation Karibu Tanzania FKT Asunta Ngatunga amesema Tangu Kituo hicho kilipoanzishwa wamefanikiwa kuwaokoa Watoto 928 waliofanyiwa ukatili ambapo kwa sasa Watoto 25 pekee wapo Kituoni
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Mwanza SP Virginia Sodoka ameoiomba Jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kufichua Wahalifu hasa wanaofanyia Watoto vitendo vya ukatili
Msaada huo wa mahitaji maalum kwa Watoto hao waliofanyiwa vitendo vya ukatili umetolewa kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani .